Pages

Saturday, July 23, 2022

MNMA YATUMIA MAONESHO VYUO VIKUU KUONESHA UBUNIFU WA TEKNOLOJIA KUTATUA CHANGAMOTO KATIKA JAMII


Mbunifu wa Teknolojia ya Kuangalia Wafanyakazi wanatoa huduma katika Vituo vya Mafuta wa Kampasi ya Karume -Zanzibar ya Chuo cha Kumbukukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) Yusuf Abbas akionesha mfumo unavyofanya kazi katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Mbunifu wa Teknolojia ya Kuangalia matumizi ya Gesi Majumbani Kampasi ya Karume-Zanzibar ya Chuo cha  Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA)  Warda Hamduni Mjomba  akionesha mfumo unavyofanya kazi katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Mbunifu wa Teknolojia ya  kuwasha pikipiki kwa kutumia alama za vidole akionesha tekonolojia hiyo itayopunguza wizi wa pikipiki wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA)  Eliza Semuowo  katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

CHUO cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  (MNMA) kimekuwa katika kuendeleza ubunifu wa wanafunzi katika Teknolijia zinazokwenda kutatua changamoto kwenye jamii.

Katika maadhimisho ya Wiki ya Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja chuo hicho kimekuja na wanafunzi ambao wamefanya ubunifu mbalimbali.

Kwa mujibu wa Chuo hicho kinaeleza wazi wanafunzi ambao wanaomba maombi chuo hicho wanatakiwa kujua ubunifu wa mwanafunzi hautaishia katika ndoto yake kichawani.

Chuo hicho kimekuwa katika program mbalimbali za kozi na wanafunzi wanaopita chuoni hapo  wanakuwa na weledi pale wanapohitimu na hata wanapojiari au kuajiriwa weledi huo silaha katika kuleta maendeleo ya nchi.

Akizungumza katika mahojiano Maalum na Michuzi TV, Mbunifu wa Kampas ya Karume- Zanzibar  ya Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Yusuf Abbas Salehe anasema kwenye Maonesho hayo amekuja ubunifu wa kifaa ambacho katika vituo vya mafuta mfumo utamuona mfanyakazi anapoweka mafuta kwenye vyombo vya moto baada ya kuingizwa katika mfumo huo.

Amesema kuwa mfanyakazi anapoingia kazini lazima aingize nywila (paswad) yake na kumruhusu kufanya kazi na msimamizi wa kituo kuwajua wafanyakazi wake.Kupitia mfumo wa ubunifu huo mmiliki wa kituo anaweza kujua idadi za lita za mafuta zilizouzwa kwa kila mfanyakazi wa kituo.

Kwa upande wake Mwanafunzi wa Chuo hicho Kampasi ya Karume  ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  Warda Hamduni Mjomba amebuni kifaa kinachoweza kutumika kuangalia matumizi ya gesi ya majumbani lwa mtungi mdogo.

Amesema kuna changamoto kwenye matumizi ya gesi za majumbani zinaisha bila yao kujua hivyo itakuwa suluhu baada ya kukamilika kwa kufunga kifaa ambacho mtu atajua gesi inaisha lini.

Pamoja na ubunifu huo  mmoja wa wanafunzi wa Mwalimu Nyerere Eliza Semuowo amefanya ubunifu wa kifaa cha pikipiki ambacho kuwasha kwake ni kwa kutumia alama za vidole.

Amesema amebuni kutokana na  changamoto ya wizi wa pikipiki ambayo  inawaathiri vijana wa wanaojipatia kipato kupitia  pikipiki (Bodaboda) hivyo wakiwa na mfumo huo kuibiwa itakuwa vigumu kuwani kuwasha kwake  lazima alama za vidole ihusishwe.

No comments:

Post a Comment