Pages

Monday, July 11, 2022

Teknolojia Itakayoboresha Mifumo Tanesco Yaiva

 Nelson Kimaro, Mtafiti Msaidizi wa Mradi wa Umeme Janja, akionyesha mfumo huo unavyofanya kwenye kompyuta ambayo itakuwa kayiam ofisi za Tanesco, kwa wadau (hawaonekani) waliofika katika banda lao lililopo katika Maonyesho ya biashara  ya Kimataifa, Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaaam leo Julai 11, 2022


Na Karama Kenyunko Michuzi TV

WAKATI Teknolojia ya Sayansi na Mawasiliano inazidi kupamba moto nchini tayari Chuo Kikuu cha Dar es Salaam College of information and communication Technology Co ICT, wamekuja na utafiti uliobuni 'umeme Janja utakaosaidia kurahisisha utoaji wa taarifa kwa Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco) kuhusiana na matatizo ya Transofoma.

Akizungumza na Michuzi Blog, leo Julai 10, 2022, Dar es Salaam, katika maonyesho ya 46 ya Kimataifa, Sabasaba, Nelson Kimaro, Mtafiti Msaadizi wa mradi huo amesema mradi huo unaofanywa chini ya chuo Kikuu cha Dar Es Salaam pamoja na Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco) unalenga kuboresha mifumo ya usimamizi ya Transfoma.

“Mradi huu unalenga kuboresha mifumo ya usimamizi wa Transfoma za Tanesco na kwamba ikitokea Transfoma ikapata tatizo ama la kulipuka ama kuishiwa mafuta au tatizo lolote lile, basi mfumo huu utaweza kupeleka taarifa moja kwa moja Tanesco kujulisha kuwa sehemu fulani Transfoma imepata tatizo la aina gani bila ya kusubiri mpaka mwananchi apige simu kupeleka taarifa," amesema Kimario.

Amesema mradi huo unalenga kuboresha zaidi mifumo ya usimamizi wa transfoma za Tanesco hususani pale inapotokea shida katika transfoma za mitaani na kusaidia kuharakisha matengenezo na marekebisho ya umeme pale panapotokea hitirafu.

“Mradi huu unalenga kutatua tatizo pale linapotokea tatizo linalohusiana na transfoma kule mitaani  muda huo huo unatoa taarifa kwa Tanesco kwamba ni tatizo gani limetokea na ni katika transfoma gani, na siyo mpaka kumsubiri mtu apige simu ya kutoa taarifa

Ameeleza namna mfumo huo utakavyofanya kazi amesema kuwa kutakuwa kuna kifaa maalum kitachofungwa kwenye Transfoma kitakachotuma ujumbe maalamu kwa wataalam wa Tanesco kwenye mfumo wa Kompyuta zikatazofungwa kwenye ofisi za Tanesco.

Amesema kuwa mradi huo upo hatua za mwisho kukamilika na tayari walishapeleka Dodoma ambapo mfumo ulifanya kazi vizuri.

Hadija Mbambati, Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam amesema utafiti huo umewahusisha wanafunzi 11 kwenye kitivo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano( ICT)

Mbambati amesema kuwa utafiti huo umegharimu kiasi cha shilling Bilioni 7 ilkiwemo na kuwasomesha wanafunzi walioshiriki kwenye utafiti ambapo utafiti huo umefanyika kwa miaka mitano.

Amesema kuwa gharama hizo ni pamoja na kuwasomesha wanafunzi.

Nelson Kimaro, Mtafiti Msaidizi wa Mradi wa Umeme Janja, akionyesha mfumo huo unavyofanya kazi kwa wadau (hawaonekani) waliofika katika banda lao lililopo katika Maonyesho ya 46 ya biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaaam.
Nelson Kimaro, Mtafiti Msaidizi wa Mradi wa Umeme Janja, akionyesha mfumo huo unavyofanya kwenye kompyuta ambayo itakuwa kayiam ofisi za Tanesco, kwa wadau (hawaonekani) waliofika katika banda lao lililopo katika Maonyesho ya biashara  ya Kimataifa, Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaaam leo Julai 11, 2022.
 

No comments:

Post a Comment