Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania, Mhe. Donald Wright wakati Balozi huyo alipomtembelea Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya masuala waliyozungumza na kubadilishana mawazo ni pamoja na suala la Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe Jaji Dkt. Eliezer Feleshi akiagana na Bw. Kadari Singo Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute. Bw. Singo na Ujumbe wake walifika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Mtumba, Dodoma na kisha kuwa na mazungumzo.
Mmoja wa wageni waalikwa akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Kikanda cha Kupambana na Ugaidi (The Sourthen African Development Community Regional Counter Terrorism Center) ( SADC- RCTC) Hafla ya uzinduzi wa kituo hicho ilifanyika Jijini Dar Es Salaam mwanazoni mwa wiki hii .
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt, Eliezer Feleshi akiwa katika picha ya pamoja mara ya baada ya mazungumzo yao na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Bw. Sunjay Rughani aliyefuatana na Bw, Walarick Nittu Mwanasheria na Katibu wa Benki hiyo. Bw. Rughani alimtembelea Mhe. AG ofisini kwake Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment