Pages

Friday, February 4, 2022

SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA NA KUWEKA MAZINGIRA BORA NA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaudi Kigahe (Mb.) amesema Serikali itaendelea kuboresha na kuweka mazingira bora na wezeshi kwa wawekezaji na wafanyabiara nchini ili kukuza uchumi shindani na viwanda kwa maendeleo ya Taifa na kwa wananchi kwa ujumla.

Akitoa taarifa hiyo ya utekekezaji wa bajeti ya Wizara kwa wajumbe wa kamati hiyo, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Alfred Mapunda alisema katika utekelezaji wa bajeti hiyo, Wizara imepata mafanikio mengi ikiwemo uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na biashara, uanzishaji wa kongani za viwanda, uboreshaji wa masoko ya mipakani, utoaji wa huduma kwa njia ya mtandao na kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya nchi, kikanda na kimataifa.

Mhe. Kigahe ameyasema hayo wakati wa utoaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara pamoja na Taasisi zake kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Februari 3, 2022 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Akitoa majumuisho ya maoni na mapendekezo ya wajumbe wa kamati hiyo, Mhe. Kigahe amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira bora na kuwalinda wawekezaji na wafanyabiasha ili waweze kukua na kushindana na masoko ya kikanda na kimataifa pamoja na kuwawezesha kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyosaidia nchi kujitosheleza kwa bidhaa muhimu mbalimbali kama Sukari.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Makiposa(Mb.) amesema Wizara inatakiwa kuendelea kuboresha na kuweka mazingira bora na wezeshi kwa wawekezaji na wafanyabiashara, kupanua uwigo wa upatikanaji wa hiduma hadi vijijini pamoja na kusimamia uzalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini kwa kitumia malighafi za ndani ili kukuza uchumi wa nchi.

Naye, Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Erick Shigongo (Mb) ameishauri Wizara kuanzisha mfuko wa ubunifu nchini (Tanzania Innovation Fund) kwa lengo la kulea, kuendeleza na kukuza vijana wabunifu wa bidhaa mbalimbali ambazo zinaweza kuanzisha viwanda vikubwa vya uzalishaji vitakavyoongeza pato la Taifa na ajira nchini.



Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha utekelezaji wa jitahada mbalimbali katika kuendeleza Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ikiwemo kuboresha mifuko ya kuwezesha Wajasiliamali, Kulinda wazalishaji wa ndani, kutafuta masoko ya uhakika ya mazao nje ya nchi, kutoa elimu kwa umma na kuongeza ubunifu katika kitumia malighafi zinazopatikana nchini katika kutengeneza bidhaa mbalimbali nchini.

Naye, Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Erick Shigongo (Mb) ameishauri Wizara kuanzisha mfuko wa ubunifu nchini (Tanzania Innovation Fund) kwa lengo la kulea, kuendeleza na kukuza vijana wabunifu wa bidhaa mbalimbali ambazo zinaweza kuanzisha viwanda vikubwa vya uzalishaji vitakavyoongeza pato la Taifa na ajira nchini.

No comments:

Post a Comment