Pages

Wednesday, February 2, 2022

MAREKANI YAAHIDI KUTOA DOLA MILIONI TANO KWA SERIKALI YA TANZANIA KUBORESHA SEKTA YA AFYA

 




Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu leo tarehe 02 Februari, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Donald Wright.
Katika kikao kilichofanyika katika  za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.



Katika kikao hicho wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya kwa kuainisha vipaumbele vyao katika eneo la afya kinga hususani eneo la mama na mtoto, lishe, masuala  ya chanjo, kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kusisitiza uhamasishaji wa elimu ya afya kwa umma.

Waziri Ummy amebainisha kuwa kwa kutumia mfumo wa jamii shirikishi katika utoaji wa huduma ya chanjo ya UVIKO-19 maeneo ya  huduma za umma utasaidia kuwafikia watanzania wengi kupata chanjo.

Kwa upande wake Balozi Wright amesema ushirikiano uliopo baina ya nchi yake na Serikali ya Tanzania ameahidi kutoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 5 kwa Serikali ya Tanzania ili kufanikisha mpango mpya wa Global Vaccines wenye lengo la kuongeza upatikanaji wa chanjo nchini ili kuwalinda watanzania na maambukizi dhidi ya Uviko-19.

Mbali na hayo Balozi Wright ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa namna inavyokabiliana na ugonjwa wa UVIKO-19 kupitia kuelimisha wananchi kuchukua hatua stahiki zinazoshauriwa na wataalam.

Aidha Waziri Ummy ameishukuru Serikali ya Marekani kwa ushirikiano wa muda mrefu na ameahidi kuimarisha zaidi ushirikiano kwa faida ya nchi zote mbili.


No comments:

Post a Comment