Pages

Tuesday, February 1, 2022

IMEELEZWA ASILIMIA 10 KATI YA 86 YA MIRADI INAYOBUNIWA NA VIJANA NDIO INAYODUMU

IMEELEZWA kuwa kati ya asilimia 86 ya mawazo ya miradi ya kimaendeleo inayoibuliwa na vijana nchini Tanzania ni asilimia 10 pekee ya mawazo hayo ndio ambayo yamekuwa yakitekelezwa na kuleta mafanikio kwa walioibua mawazo hayo .

Kuwa sehemu kubwa ya mawazo yanayoibuliwa yamekuwa hayana mafanikio kutokana na wahusika kuibua kuibuka na mawazo ya miradi wasiyoweza kuisimamia zaidi ya kuibua kwa hisia za tamaa toka kwa wengine.

 NA Mwandishi Wetu , Mufindi


IMEELEZWA kuwa kati ya asilimia 86 ya mawazo ya miradi ya kimaendeleo inayoibuliwa na vijana nchini Tanzania ni asilimia 10 pekee ya mawazo hayo ndio ambayo yamekuwa yakitekelezwa na kuleta mafanikio kwa walioibua mawazo hayo .



Kuwa sehemu kubwa ya mawazo yanayoibuliwa yamekuwa hayana mafanikio kutokana na wahusika kuibua kuibuka na mawazo ya miradi wasiyoweza kuisimamia zaidi ya kuibua kwa hisia za tamaa toka kwa wengine.

Akitoa mafunzo ya ujasiliamali jana katika Ukumbi wa Fox Igoda Mufindi ,Mwezeshaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana waliopo katika mradi wa Youth Agency Mufindi(YAM) John Kalolo alisema kuwa tamaa ya baadhi ya waibuaji wa miradi ya kimaendeleo imekuwa ikipelekea miradi hiyo kutofanikiwa kutokana na kutokuwa na malengo sahihi ya uendeshaji wa miradi hiyo .

Hivyo alisema lazima vijana ambao wanahitaji kufanikiwa katika uibuaji wa miradi na uandishi wa miradi ni lazima kwanza kuwa ari ya kuisimamia na kuifanya miradi husika kwa kutanguliza kipaji cha uendeshaji wa miradi husika na sio kufanya kwa kuiga kwa wengine.

" Kwenye maisha wengi waliofanikiwa ni wale ambao wanafanya shughuli ambazo wanazipenda kutoka moyoni na sio wale ambao wanafanya miradi ya kuiga kutoka kwa wengine ama kwenda kuandika andiko la mradi ambao huna uwezo nao kuufanya amini utashindwa kufika mbali katika mradi wako " alisema

Serikali na wadau mbali mbali wamekuwa wakitenga fedha kwa ajili ya kuwezesha vijana na kati ya fedha hizo ni pamoja na fedha zinazotolewa na Halmashauri za wilaya nchini kupitia makusanyo yake ya ndani ambapo vijana wametengewa asilimia 4 kati ya asilimia 10 zinazotolewa na Halmashauri nchini.

Hivyo iwapo vijana watakimbilia kuandika miradi ama kuanzisha vikundi bora mradi wapate fedha hizo ndio mwanzo wa vikundi ama miradi husika kufa kabla ya kufika mbali.

Pia alisema baadhi ya vijana wameshindwa kufanikiwa katika maisha kutokana na kutanguliza imani potofu hata baadhi yao kutegemea nguvu za giza na kujikuta wanaingia katika mikono ya sheria kwa kudanganywa na waganga kwenda kufanya vitendo vya mauwaji ama vitendo viovu kwenye jamii ili kupata utajiri wa haraka haraka.

Zilipa Mgeni ni meneja mradi wa YAM alisema lengo la mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha vijana zaidi ya 770 wakiwemo watoto 150 kutoka kata tatu za Ihanu , Mdabulo na Luhunga kama ambazo zote zitaunganishwa na vijiji 16 za mradi huo .

Washiriki wa mafunzo hayo Kelvin Mnyamka na Zelida Deule mbali ya kupongeza mradi huo wa YAM kwa kuwaunganisha katika mradi huo bado walisema mfunzo hayo ni fursa kubwa kwao kusonga mbele katika shughuli za kiujasiliamali kwani awali walikuwa nyuma kutokana na kutawaliwa na mawazo potofu .


No comments:

Post a Comment