Pages

Tuesday, January 4, 2022

Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali

 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo Januari 4,2022 ameteua viongozi mbalimbali. Mheshimiwa Rais amemteua Dkt.Baghayo Abdhalah Saqware kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).

 ni Mhadhiri Mwanzamizi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA). Pia Mheshimiwa Rais Samia amemteua, Bw.Charles Jackson Itembe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Eneo Maalumu la Mauzo ya Nje (EPZA).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Bw.Itembe ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania (Azania Bank Limited).

Uteuzi mwingine ni wa Bw.Ernest Maduhu Mchanga ambaye Mheshimiwa Rais Samia amemteua kuwa Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC).

Bw.Mchanga ni Katibu Msaidizi,Fedha na Utawala, Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC) kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu kupitia taarifa aliyoitoa leo Januari 4,2022 ameeleza kuwa, uteuzi huo umeanza Januari Mosi,2022.


No comments:

Post a Comment