Pages

Monday, November 29, 2021

JUKWAA LA UBUNIFU LA SWAHILI LAUNGANA KUSHEREHEKEA MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA

Muasisi wa jukwaa la ubunifu la "Swahili fashion week" Mustafa Hassanali akizindua rasmi jukwaa hilo kwa Msimu wa 14 na akisisitiza kuungana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kusherehekea Miaka 60 ya uhuru wa Tanzania.
Picha ya pamoja  Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (Basata) akiwa pamoja na  wadhamini wa jukwaa la "Swahili fashion week"  pamoja na Muasisi wa jukwaa hilo Mustafa Hassanali wakikamilisha uzinduzi wa jukwaa hilo katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
Miongoni mwa wabunifu ambao watashiriki jukwaa la "Swahili fashion week" katika Msimu huu wa 14 tangu kuanzishwa kwake chini ya Muasisi na Mbunifu Mkongwe nchini Mustafa Hassanali.


 Na Khadija Seif, Michuzi TV

MAONYESHO ya Jukwaa la   “Swahili Fashion Week” Kwa zaidi ya Miaka 14 yanatarajiwa kufanyika Desemba 3, 4 & 5, mwaka huu katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi Wahabari Muasisi wa jukwaa la “Swahili Fashion "  Mustafa Hassanali amesema ana  matumaini ya kuimarisha msingi wa ubora wa jukwaa hilo na kwa shauku kubwa anasema Lengo la kuendeleza tasnia ya ubunifu Afrika bado linabaki kuwa kipaumbele, kupitia jukwaa hili na mtandao wake mkubwa wa vyombo vya habari, watumiaji wa bidhaa za ubunifu wa Tanzania, Afrika na ulimwengu kwa ujumla sasa wataona mbadala wa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje.

Mustafa amesema zaidi ya wabunifu sitini (60) wataonyesha vipaji vyao katika jukwaa hilo jijini Dar es Salaam Huku akisisitiza jukwaa hilo Swahili  inaungana na serikali kusherehekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

"Jukwaa kubwa la Maonyesho ya mavazi Afrika la jukwaa la ‘Swahili Fashion Week' limepanga kufanya Maonyesho yake Desemba 3, 4 na 5 mwaka huu, katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Maonyesho haya ya kumi na nne ya “Swahili Fashion Week" yataendelea kuwa kioo kwa maonyesho mengine ya mavazi Afrika kwa wabunifu wa Kitanzania, ukanda wa Afrika Mashariki hata wale wa kimataifa kwa mvuto na mandhari yake ya kipekee inayoendana na kauli mbiu ya jukwaa ya Tambua Kinachoipendezesha.

Jukwaa la  "Swahili Fashion Week" inashirikiana na Serikali na wananchi kusherekea miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara ikiwa na dhamira ya kuonyesha ubunifu wa kupendeza, ubora na uzuri wa nchi, ili kuitangaza na kuongeza uchumi.

Jukwaa pia linawahimiza wabunifu wachanga kutumia jukwaa hili, ikiwa ni hatua moja wapo katika kukuza vipaji vyao vya ubunifu kwa mara nyingine kutakua na shindano la wabunifu chipukizi linalojulikana kama “Washington Benbella Emerging Designers Competition” ambapo wabunifu 10 wanatarajiwa kuonyesha umahiri wao kwenye ubunifu kupitia jukwaa hili.

No comments:

Post a Comment