Na.WAMJW,Dodoma
Watumishi wa huduma ya afya nchini wametakiwa kufuata maadili sahihi ya taaluma zao wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa wateja wanaofika kwenye vituo vya afya.
Hayo yamesemwa mapama leo Oktoba 29, 2021 na Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasiliamali Watu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Saitori Laizer, wakati wa kuwajengea uwelewa wahitimu wa maabara wa vyuo mbalimbali
ambao wanaanza mafunzo kwa vitendo(watarajali) kwenye hospitali hapa nchini.Amesema katika sekta ya afya kuna maeneo mawili ambayo mtoa huduma anapaswa kufahamu kwanza kabisa nidhamu kazini, lakini pia usiri kwa wagonjwa juu ya vipimo mnavyo vichukua mhakikishe majibu yake yanakua siri kati ya mteja na mtoa huduma.
“Baadhi ya watu mmekuwa na tabia za ajabu sana kwenye vituo vyenu utakuta mgonjwa anakuja kupatiwa matibabu halafu baadae utamkuta mtu wa maabara anaanza kutoa siri za vipimo vya wagonjwa hilo suala sio la misingi ya taaluma ya kada za Afya”.Aliendelea
”ifikie kipindi jamii ifurahie na huduma mnayo itoa pindi mkiwa katika vituo vya afya kwani maadili ya kazi ndiyo huleta matumaini kwa wagonjwa mnao wahudumia mfano mzuri nyie wenye taaluma nyeti ya vipimo maana mgojwa kabla ya kupata matibabu lazima apitie kwenu ili kufahamu njoo gani mtaitumia kumsaidia”. Alisema Dkt. Laizer
Kwa upande wake Msajili wa Baraza la Watalamu wa Maabara, Mary Mtui, amesema takribani watarajali 275 wamepangwa katika vituo 21 vilivyo ainishwa na Baraza la Afya nchini, aliendelea kuwa hadi saa tangu wafungue vituo hivyo vya mafunzo kwa watarajali hawajawahi kupokea kesi yoyote ya mtarajali ambaye ameshindwa kufuata maadili ya kazi pindi akiwa kituoni.
Aidha, Mary alisisitiza kuwa baraza limekuwa na tabia ya kupata mrejesho kutoka kwa watarajali mara mbili katika vituo vya mafunzo ili kufahamu utekelezaji wa mafunzo yao ya utarajali.
“Tumekuwa tukifanya hivyo ili kufahamu changamoto Wanazo kutana nazo watarajali pindi wakiwa kwenye mafunzo hayo na sisi kama Baraza tunahakikisha tunatatua changamoto hizo ili kuendelea kutoa huduma sahihi ya elimu kwenye vituo vyetu”. Alisema.
Akizungumza katika hafla hiyo Spika mstaafu wa baraza la wawakilishi Zanzibar, Pandu Amir Kificho, aliwataka watarajali hao kufuatilia taarifa mbalimbali katika mitandao ili kuweza kujifunza zaidi na kuweza kuimarisha taaluma zao na sio kusubiri mafunzo toka vyuoni.
Amesema wimbi kubwa la watanzania huja katika vituo vya afya ili kupatiwa huduma kulingana na matatizo waliyo nayo, hivyo tumieni kama nafasi ya kubadili huduma zenu ziwe faraja kwa wateja wenu.
No comments:
Post a Comment