Pages

Saturday, July 31, 2021

WAZIRI BITEKO AIPONGEZA SHANTA GOLD KWA KUSIMAMIA LOCAL CONTENT

Waziri wa madini Doto Biteko akizungumza na uongozi wa Mgodi wa Kati wa Dhahabu wa Singida (SINGIDA GOLD MINE) Shanta uliyopo wilaya ya Ikungi Mkoani Singida alipotembembelea  na kukagua Maendeleo ya ujenzi  wa mgodi huo tarehe 30 Julai, 2021 Ikungi Mkoani Singida

Meneja Mkuu Mahusiano ya Serikali wa mgodi wa Shanta, Philibert Rweyemamu akiwasilisha tarifa ya Maendeleo ya ujenzi wa mgodi huo kwenye ziara ya Waziri Biteko tarehe 30 Julai, 2021 Ikungi Mkoani Singida

Mkuu wa Mkoa wa Singida Binilith Mahenge akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Madini Doto Biteko kwenye ziara ya kutembelea mgodi wa Shanta na shughuli za uchimbaji wa Dhahabu mkoani Singida tarehe 30 Julai, 2021

………………………………………………………………………..

Na. Steven Nyamiti – Singida

Waziri wa Madini Doto Biteko ameeleza kuwa, Mgodi mpya wa Kati wa Dhahabu wa Shanta ndio mgodi pekee Tanzania unaotekeleza ipasavyo Matakwa ya Sheria ya

matumizi kwa Jamii husika (Local Content).

Amesema hayo tarehe 30 Julai, 2021 alipotembelea na kukagua Maendeleo ya ujenzi  wa Mgodi wa Kati wa Dhahabu wa Singida (SINGIDA GOLD MINE) Shanta uliyopo wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.

Amesema historia ya ujenzi wa mgodi huo, kwa miaka mitano yote iliyopita Mgodi wa Shanta ndio mgodi wa Kati mpya uliojengwa hapa Nchini.

Akizungumzia kuhusu umuhimu wa Sheria ya Local content amesema kuwa, katika uwekezaji inawahitaji wakubwa, wa kati na wadogo ili kufanya uchumi uwe na maana.

“Kama biashara wafanye wenyeji, tulikuwa na migodi ambayo hata nyama ilitoka South Africa, lakini mgodi ambao mwaka huu tumewapa tuzo ya Local content, huu ndio mgodi ambao asilimia 100 ya walioajiriwa ni watanzania,”ameeleza Biteko.

Aidha, ameipongeza kampuni ya uchimbaji madini ya Shanta kwa kupiga hatua katika kusimamia Sheria hii ya Local content  na manunuzi ya bidhaa katika migodi yao kwa asilimia kubwa ambao unategemea kuanza  shughuli za uzalishaji wa dhahabu Mwezi Novemba 2022.

Naye, Meneja Mkuu Mahusiano ya Serikali wa mgodi wa Shanta, Philibert Rweyemamu amemueleza Waziri Biteko kuwa, wanashirikiana na uongozi wa Wilaya na Mkoa katika kutoa kipaumbele katika shughuli za maendeleo. Amesema wananchi wa Ikungi na Singida kwa ujumla  wanapata ajira mbalimbali zinazotolewa na mgodi huo pamoja na  manunuzi ya bidhaa mbalimbali.

Pia, Meneja Mkuu Shanta Mradi wa Singida Jiten Divecha akisoma taarifa ya mgodi huo ameeleza kuwa,   hadi sasa mgodi unawafanyakazi 117 sawa na asilimia 70 ambao wameajiriwa kutoka vijiji vinavyozunguka  mgodi.

“Tumekamilisha vyumba vya madarasa ya shule ya Sekondari Mangonyi Shanta na madawati 183,” amesema Divecha.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Singida Binilith Mahenge ameipongeza Serikali  kupitia wizara ya madini kwa mageuzi  makubwa katika sekta ya madini hapa nchini. Amesema  mageuzi ni mengi makubwa  na utunzaji wa rasilimali madini.

“Shanta sina wasiwasi nao, sisi kama wasimamizi wa mkoa huu tutakuwa pamoja katika kusimamia mgodi huu katika kuimarisha usalama na niwahakikishie fanyeni kazi, hatutakuwa sehemu ya changamoto bali tutatatua changamoto zenu. Kuhusu miundombinu ya barabara na maji nitahakikisha kama Mkuu wa mkoa vinapatikana hapa,” ameongeza Mahenge.

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Rajab Mtaturu amemueleza waziri Biteko kuwa, mgodi huo wa Shanta utachochea shughuli za uchumi kwa wananchi  baada ya mgodi kuanza kufanya kazi. Amesema yeyé kama muwakilishi wa wananchi wa Singida Mashariki anatamani mgodi uanze shughuli za uchimbaji haraka ili kurahisisha maendeleo.

Waziri Biteko amefanya ziara ya kutembelea Mgodi wa Marwa Marwa and Partiners, Kukagua shughuli za uchimbaji na kuzungumza na Wachimbaji Wadogo katika kijiji cha Sambalu kata ya Mangonyi wilaya ya Ikungi. Biteko amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jery Muro na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida kuhakikisha wanafungua Vituo vya kununulia Dhahabu katika eneo la mgodi ili kurahisisha wachimbaji wadogo kupata huduma kwa haraka.

 

No comments:

Post a Comment