Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe Dkt. Faustine Ndugulile na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe, Innocent Bashungwa wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo cha kurushia matangazo cha TBC Taifa na TBC FM kilichojengwa kwa ufadhili wa UCSAF. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC,Dkt. Ayub Rioba na wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo cha TBC katika kijiji cha Sesenga, wilayani Morogoro, Mkoani Morogoro. Kituo hicho kimefadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote( UCSAF).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo cha TBC katika kijiji cha Sesenga, wilayani Morogoro, Mkoani Morogoro.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF), Justina Mashiba akisaini hati ya makabidhiano ya kituo cha kurushia matangazo cha TBC Kisaki kilichojengwa kwa ufadhili wa Mfuko huo.
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe, Dkt Faustine Ndugulile amesema Wizara yake imejielekeza katika kumaliza kabisa tatizo la usikivu wa radio na simu katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo maeneo ya pembezoni na mipakani mwa nchi ifikapo mwaka 2025.
Waziri Ndugulile ameyasema hayo katika
uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo ya TBC Taifa na TBC FM
kilichopo katika kijiji cha Sesenga, wilayani Morogoro, Mkoani Morogoro,
kituo kilichojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote
(UCSAF) kwa lengo la kuboresha usikivu wa radio katika eneo hilo na
maeneo ya jirani ikiwemo eneo la kimkakati katika bwawa la kuzalisha
umeme la Mwalimu Nyerere.
Amesema hadi sasa asilimia 66 ya maeneo
ya kijeografia nchini yanapata huduma ya mawasiliano lengo likiwa ni
kufikia asilimia 100 ifikapo mwaka 2025. Kwa upande mwingine amesema
matumizi ya intanet kwa sasa ni asilimia 43 lengo ni kufikia asilimia
100 pia ifikapo 2025. Kwa upande wa usikivu wa radio tayari Wizara
kupitia UCSAF imetangaza zabuni ya kupeleka mawasiliano katika kata 190
zilizo maeneo ya mipakani.
Ili kuboresha mawasiliano ya simu na
huduma zingine za utangazji katika eneo hilo, Waziri Ndugulile ameiagiza
UCSAF kufanya mazungumzo na makampuni ya simu pamoja na watoa huduma za
utangazaji kutumia mnara huo mpya kuwekeza katika eneo hilo ili
kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora za mawasiliano ya simu na
utangazaji.
Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe, Innocent Bashungwa ameipongeza Wizara kupitia Mfuko wa Mawasiliano
kwa Wote kwa kutekeleza kwa vitendo ilani ya CCM ya 2021-2025 kwa
kuiwezesha TBC kupata vifaa vya kisasa vitakavyoisadia kupanua na
kuboresha usikuvu wa radio za TBC nchi nzima.
Akizungumza kwa
niaba ya Kamati ya Bunge ya kudumu ya Miundombinu, Mhe. Innocent
Karogenis amesema Kamati inazopongeza wizara hizo mbili kwa kushirikiana
katika kuzingatia mapendekezo yanayotolewa na Kamati.
Mtendaji
Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba asema kuwa, UCSAF imetoa shilingi milioni
450 kujenga kituo hicho cha kurushia matangazo na ununuzi wa vifaa vya
kisasa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya Mfuko katika
kuhakikisha mawasiliano, yakiwemo matangazo ya redio yanafika kwa watu
wote nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba amesema
kuwa ujenzi wa kituo hicho cha kurushia matangazo utakuwa na manufaa kwa
wanananchi wa maeneo hayo pamoja na maeneo mengine ikiwemo mbuga ya
Selous kwa kuwa wataanza kupokea matangazo ya TBC Taifa na TBC FM.
No comments:
Post a Comment