Mkuu
wa Jeshi la Nchini (IGP) Simon Sirro akizungumza kuhusiana na Shirika
la Uzalishaji Mali la Jeshi Polisi kuingia katika Uwakala wa Bima katika
hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu
Mwenyekiti wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi Polisi (TPFCS ) Toyi
Ruvumbagu akizungumza kuhusiana na utekelezaji wataofanya katika
kuhudumia Jeshi hilo katika Bima .
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dk.Elirehema Doriye
akizungumza kuhusiana na utendaji wa Shirika katika kuwafikishia
watanzania huduma za Bima zilizo katika hafla ya kuingia makubaliano
Kati NIC na Jeshi la Polisi.
*NIC yaahidi kuendelea kutoa huduma bora za Bima
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MKUU
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amelitaka Shirika la Bima la
Taifa (NIC) kuhakikisha linatoa elimu ya kutosha kwa jeshi la polisi
kuhusu umuhimu wa kuwa na bima za maisha ili kuwezesha askari wengi
kujiunga na huduma hiyo kwa maana wapo kwenye kazi hatarishi katika
kazi zao.
Akizungumza
katika hafla ya Kuandikishiana Hati ya Makubaliano hafla ya
Kuandikishina hati ya makubaliano kati ya Shirika la Taifa la Bima(NIC )
na jeshi la polisi kupitia Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi hilo ya
kuwa Wakala wa Bima iliyofanyika Makao makuu ya shirika hilo Jijini Dar
es salaam IGP Sirro amesema kuna ulazima wa shirika la bima la NIC
kutanua wigo na kuweza kuwafikia watanzania wengi waweze kupata uelewa
wa huduma za bima na kuweza kujiunga na huduma hiyo kwani inamanufaa
makubwa pia ni Shirika la watanzania.
"Vijana
wetu wamekuwa wakigongwa na magari katika kazi zao za kupitisha magali
barabarani, unamsimaisha dereva amelewa aangalii huyu ni askari polisi
anamgonga kwahiyo kuwa na bima ya maisha ni jambo la msingi sana kwani
wanakuwa wanafamilia zao zinazowategemea" Amesema IGP Sirro.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dk.
Elirehema Doriye amesema Shirika linatoa huduma zote za bima za maisha
na bima za mali na ajali, kwa kutoa huduma hizo pia inafanya huduma za
uwakala wa shirika la uzalishaji mali la jeshi la polisi kuwa na wigo
mpana zaidi kwa kuwafikia askari ndani ya jeshi.
"Kupitia
uwakala utawezesha jeshi la polisi,maafisa,wafanyakazi pamoja na
familia zao na watanzania wote kupata huduma zote za kibima kupitia
wakala washirika la uzalishaji mali la jeshi la polisi". Amesema
Dk.Doriye.
Pamoja
na hayo Dk.Doriye amesema kupitia mahusiano yao na Shirika la
uzalishaji mali la jeshi la polisi watakuwa wanaenda kutekeleza mpango
mkakati wa maendeleo ya sekta ya bima ambao kwa kiasi kikubwa utaongeza
ufahamu wa bima lakini pia utumiaji wa huduma za bima nchini.
"Kwa
sasa utimiaji wa huduma za bima ni asilimia 15 na kwa watanzania na
ili tufike mpango wa serikali ambapo kufikia mwaka 2030 asilimia 50 ya
watanzania wawe wanatumia huduma za bima lakini pia uelewa wa bima kwa
tanzania ni chini yya asiliia 40 na mpango wa serikali ni kuhakikisha
kwamba inapofika mwaka 2030 asilimia 80 ya watanzania wanaelimu sahihi
ya bima". Amesema
Hata
hivyo amesema kuwa kupitia mahusiano hayo wanaenda kutekeleza pia
mikakati ya serikali kuhakikisha kwamba kuna ukuaji kwenye sekta ya
fedha.
Nae
Makamu Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Uzalishaji Mali ya Jeshi la
Polisi (TPFCS) Toyi Ruvumbagu amesema kupitia makubaliano hayo jeshi
litanufaika na fursa kama kupata wepesi wa kufikia huduma za bima kwa
askari nchini, kumbukumbu zinaonesha kwamba idadi ya askari na maofisa
wa jeshi la polisi wanaopata huduma za bima hasa bima ya maisha iko
chini hivyo kupitia fursa hii ya shirika linakusudia kutumia mifumo ya
kijeshi kuhamasisha askari kujiunga na huduma hii
Aidha
amesema jeshi la polisi litanufaika kwa kuweza kupata bei za kimakundi
kwa bima ya afya ambayo ni group cover na kulingana na idadi ya ya
askari na maofisa watakaojiunga na bima hiyo ambao zinaunafuu
ukilinganisha na bei za kawaida za soko.
"Kwa
mfano tukipata kuunga askari mmoja mpaka askari elfu 10, tutapata
punguzo la asilimia Tano tukiweza kupata askari elfu 10 mpaka shilingi
20,000 tutapata punguzo la asilimia 7.5 tukipata askari elfu 20 mpaka
wakafika askari 30 tutapata punguzo la asilimia 10% kutoka bima yeu hii
na tukipata askari zaidi ya elfu 30 tutapata punguzo la asilimia 12 ".
Amesema Bw.Ruvumbagu.
Amesema kupitia fursa hiyo kutawezesha askari wetu kujiunga katika huduma kwa bei rafiki iwapo kundi kubwa litahamasika.
No comments:
Post a Comment