Pages

Thursday, July 1, 2021

MATUKIO KATIKA PICHA: KIKAO CHA USHIRIKIANO NGAZI YA MAKATIBU WAKUU BAINA YA OFISI YA WAZIRI MKUU NA OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS (SMZ)

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda akifungua kikao cha Ushirikiano Ngazi ya Makatibu Wakuu baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ) kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Julai 1, 2021 Jijini Dodoma, kikao hicho kililenga kujadili utekelezaji wa Shughuli za Serikali kwa pande zote mbili.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Bw. Idarous Thabiti Faini akifafanua jambo wakati wa kikao cha Ushirikiano Ngazi ya Makatibu Wakuu baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ) kilichofanyika tarehe 01 Julai, 2021 Dodoma.

Mkurugenzi wa Uratibu Sherehe za Kitaifa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bi. Riziki Daniel akichangia jambo kuhusu masuala ya uratibu wakati wa kikao cha Ushirikiano Ngazi ya Makatibu Wakuu baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ).

Mkurugenzi wa Idara ya Bunge na Siasa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Raymond Kaseko akiwasilisha taarifa kuhusu Uratibu wa Shughuli za Serikali Bungeni wakati wa kikao cha Ushirikiano Ngazi ya Makatibu Wakuu baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ) kilichofanyika Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango na Bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Vonyvaco Luvanda akiwasilisha kuhusu Muundo wa Majukumu ya Ofisi hiyo wakati wa kikao cha Ushirikiano Ngazi ya Makatibu Wakuu baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ).

Kaimu Murugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Bw. Issa M. Khamis akiwasilisha Muundo na Majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) wakati wa kikao hicho.

Baadhi ya majumbe wakifuatilia kikao kazi hicho.

Baadhi ya wajumbe wa kikao wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira  na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda wakati wa kikao hicho.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Paul Sangawe akifafanua jambo kuhusu masuala ya kuratibu Serikali kuhamia Dodoma wakati wa kikao  hicho.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda (katikati), Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Bw. Idarous Thabiti Faini (kushoto kwake), Naibu Katibu Mkuu (Sera, Uratibu  na Bunge) Bw. Kaspar Mmuya (wa pili kutoka kulia), Naibu Katibu Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Jamal Katundu (Wa kwanza kushoto) pamoja na Afisa Utumishi Idara na Shughuli za SMZ Dar es Salaam Bw. Heri Khamis Makame (wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe walioshiriki katika kikao hicho.

(PICHA ZOT NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

 

No comments:

Post a Comment