Na Khadija Seif Michuzi Tv
TAASISI ya The warrior Women yawakaribisha wajasiriamali na wapenzi wa bidhaa zao katika Maonesho ya Biashara ya Sabasaba Dar es salaam.
Akizungumza na Michuzi Tv Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Sabra Machano amesema kupitia Taasisi ya The warrior Women inalenga kuwakwamua wajasiriamali wadogo wadogo kutoka sehemu mbalimbali.
"Katika Maonesho ya Sabasaba tumeanza kutoa nafasi kwa wafanyabiashara wadogo wadogo hasa wa vyakula Kuna juice,viungo vya vyakula,urojo pamoja na bidhaa za urembo kwa ujumla."
Machano amesema kwa Sasa ameanza na wafanyabiashara wachache kadri muda unavozidi kwenda wataweza kuongeza na wafanyabiashara wengine kwa Mikoani hasa Arusha,Dodoma na Mikoa mengine.
Hata hivyo kwa upande wake Mmoja wa wajasiriamali ambao kupitia Taasisi hiyo imewapa nafasi ya kuonyesha bidhaa zao katika Maonyesho hayo Zuwena Ally maarufu kama Manju duox ambae anatengeneza bidhaa za viungo vya chakula pamoja na bidhaa za urembo.
"Ni nafasi pekee ya kutambulisha bidhaa zetu ambazo ni Bei nafuu na bidhaa Bora kuliko zote katika Maonyesho haya na inatupa fursa ya kuweza kuwafikia wateja wetu kwa haraka na kuuza kwa wakati."
Pia Manju duox ameongeza kuwa fursa kama hiyo ni muhimu kwani mbali na kupata nafasi ya kuuza bidhaa Bali pia inampa fursa mfanyabiashara kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara wengine na kutanua kimasoko zaidi.
No comments:
Post a Comment