Pages

Wednesday, June 30, 2021

SHIRIKISHO LA UWANG'MAK LAZINDULIWA LEO DAR, WAASWA KUZALISHA BIDHAA ZENYE UBORA

 

Viongozi Mbalimbali wa bodi ya Maziwa na wanavikundi 14 wanaounda shirikisho la wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa Kinondoni wakizindua shirikisho hilo leo Mkoani Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau wa shirikisho la wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa wa Kinondoni wakiwa katika uzinduzi wa shirikisho lao leo.
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya akizungumza wakati wa uzinduzi wa chama cha shirikisho la wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa Kinondoni (UWANG'MAK) leo Mkoani Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa shirikisho la wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa Kinondoni (UWANG'MAK) wakinywa maziwa wakati wa uzinduzi wa Chama cha Ushirika cha wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa Kinondoni (UWANG'MAK) leo Mkoani Dar es Salaam.

CHAMA cha Ushirika cha wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa Kinondoni (UWANG'MAK) imeiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwepo na vituo vya kukusanya maziwa hapa nchini ili maziwa kuwa na viwango vya ubora.

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa wanachama cha ushirika wa wafugaji Ng'ombe wa Maziwa wakati akiwasilisha Risala mbele ya Mgeni rasmi, Grace Ngassa wakati wa uzinduzi wa chama cha ushirika cha wana UWANG'MAK leo Juni 30,2021 katika uzinduzi uliofanyika Mkoani Dar es Salaam. Amesema licha ya kupata mafunzo katika maonesho ya nanenane lakini kunachangamoto ya ukosefu wa Ng'ombe wa kisasa.

Licha ya hayo wameomba kutengwa kwa maeneo maalumu kwaajili ya wafugaji wa ng'ombe wa maziwa wa chama cha Ushirika cha wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa Kinondoni (UWANG'MAK) ili waweze kufuga ufugaji wenye tija na ufugaji wa biashara.

Mmoja wa wanaushirika wa UWANG'MAK mesema kuwa ili kuwa na Ng'ombe wanaotoa maziwa yenye ubora ni lazima Ng'ombe aweze kula majani ya kijani mengi ili aweze kushiba na kutoa maziwa mengi.

Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya Amesema kuwa wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa wanahitaji kuzalisha maziwa mengi na yenye viwango ili kukidhi mahitaji wa watu kwani kila mwananchi anatakiwa kunywa maziwa lita 200 kwa mwaka.

Licha ya hayo amesema kuwa ni mhimu kutafuta soko la uuzaji wa maziwa kwani mnunuaji mmoja mmoja sio soko la uhakika, hivyo mtu mmoja asipo nunua italeta kharaha kwa mfugaji.

Amesema pia ni mhimu kuwa na viwanda ili kusaidia maziwa yanayozalishwa na wafugaji wa Ng'ombe wa maziwa kupata soko la uhakika na hivyo uchumi wa mmoja mmoja kukua na hatimaye uchumi wa taifa.

Licha ya hayo amewaomba wafugaji wa Ng'ombe wa maziwa wawe na Lugha moja ambayo itawasaidia katika kujikuza katika sekta hiyo mhimu na yenye utajiri mwingi wa Vitamini.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Kindondoni, Stella  Msofe amesema kuwa wanahakikisha wanapata wanashirikisho la Wafugaji wa Ng'ombe wa maziwa mazao wanayoyazalisha yawe bora na yanayokidhi vigezo vyote

"Kwa hiyo sasa turejee kujenga shirika ambalo ni imara ili liweze kusonga mbele kwaajili ya tasnia yetu ya maziwa. Amesema Stella

Chama cha Ushirika cha wafugaji wa ng'ombe wa Maziwa Kinondoni (UWANG'AMAK) Chama hicho kimeshirikisha vikundiva wafugaji Ng'ombe wa Maziwa 14 viliopo Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment