Waziri
wa Madini - Dotto Biteko (kushoto) na Afisa Mkuu wa Mikopo Benki ya NMB
– Daniel Mbotto wakizindua rasmi jukwaa la ‘NMB Mining Club’ katika
hafla ya uzinduzi iliofanyika katika hoteli ya Morena - Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB – Alex Mgeni akiwaelimisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini Kanda ya Kati waliohudhuria uzinduzi wa NMB Mining Club kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na benki ya NMB.
Benki ya NMB imeendelea kuweka
historia nyingine tena kwa kuzindua jukwaa la kwanza nchini mahsusi la
kuwahudumia wadau wa Sekta ya Madini liitwalo ‘NMB Mining Club’.
Klabu hiyo mpya imejumuisha zaidi ya wadau wa madini 200 wa Kanda ya
Kati na imelenga kutoa mafunzo kuhusu maarifa ya biashara (elimu juu ya
mipangilio ya biashara na elimu ya mwendelezo wa kitaalamu wa madini) na
fursa ya kukutana na kubadilishana uzoefu wa kibiashara.
Wadau
hao ni pamoja na wamiliki wa migodi, maduka makubwa ya vifaa vya
uchimbaji, viongozi kutoka kampuni za madini, Kampuni ya Taifa ya Madini
(Stamico), vyama vya wachimbaji wa kada zote na madalali.
Mgeni
rasmi katika uzinduzi wa jukwaa hilo uliofanyikakatika hoteli ya
Morena- Dodoma, Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko aliwapongeza NMB kwa
ubunifu huo wa kuwafikia na kuwaunganisha wadau wa Sekta hiyo huku
wakiwapa fursa ya mafunzo ya biashara na kubadilishana mawazo kwa ajili
ya ufanisi wao binafsi na kisekta kwa ujumla.
Mhe.Biteko,
amewahakikishia wawekezaji na wadau wengine wa sekta ya madini mazingira
bora ya uwekezaji na kufanya biashara akisema hicho ni kitu muhimu kwa
ustawi wa sekta hiyo na maendelo ya taifa kwa ujumla.
Awali,
Afisa Mkuu wa Mikopo wa NMB, Bw. Daniel Mbotto, alisema mafunzo hayo
yamekuja wakati biashara nyingi zikipata changamoto akitolea mfano wa
kushuka kwa thamani ya bei ya Tanzanite kwenye soko la dunia.
Kuhusu
“NMB Mining Club”, Bw. Mbotto alisema ni mpango unaolenga kufikia miji
sita nchini yaani Mwanza, Chunya, Morogoro na Arusha, ukianzia Dodoma na
Kahama na maeneo ya karibu kwa lengo la uwezeshaji na kutoa mafunzo ya
biashara. Ubunifu huu ndio unaoifanya NMB kuendelea kuwa kinara wa
huduma na bidhaa katika sekta ya kibenki.
No comments:
Post a Comment