Raia saba wa Iran walokamatwa Aprili 23,2021 mkoani Lindi akisafirisha dawa za kulevya.
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
RAIA
saba wa Iran wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi wa
wakikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine
na Methamphetamine zenye uzito wa jumla ya kilo 859.36
Katika
hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali
Mwandamizi Joseph Maugo akisaidiana na wakili Mwandamizi Juma Maige
imewataja washtakiwa hao kuwa ni,
Jan
Mohammad Miran, Issa Baluchi Ahmad, Amir Hussein Kasom, Salim Baluchi
Fedhmuhammad, Ikbal Pakil Mohammad, Mustapha Nowan Kadir Barkshi na
Jawid Nuhanur Nur Mohammad.
Kesi hiyo ya uhujumu namba 02 ya 2021 imesomwa leo Aprili 30,2021 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Maria Bantulayne.
Akisoma
hati ya mashtaka wakili Maugo amedai, Aprili 23, 2021 huko katika
Bahari ya Hindi mkoa wa Lindi ndani ya eneo la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania, washtakiwa walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya
Herione zenye uzito wa kilo 504.36.
Imeendelea
kudaiwa kuwa siku na mahali hapo, washtakiwa hao pia walikamatwawa
wakisafirisha dawa zingine za kulevya aina ya Methamphetamine zenye
uzito wa kilo 355 kinyume cha sheria.
Hata
hivyo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya
Uhujumu uchumi.
Kwa
mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado
haujakamilika na kesi hiyo imepangwa kutajwa tena Mei 14 2021
washtakiwa wamerudishwa rumande.
No comments:
Post a Comment