Mkurugenzi
Mtendaji wa kituo hicho, Theodosia Muhulo (wa pili kutoka kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam leo Aprili 30,
2021. Wakwanza kushoto ni Katibu wa wafanyakazi SBS, Crement Bundi,
Kutoka Kulia ni Sekela Kanamela na wapili kulia ni Mwalimu Bhoke Makulu.
Katibu wa wafanyakazi SBS, Crement Bundi akizungumza na waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam leo.Sekela Kanamela wa kwanza kulia akizungumza na waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam leo.
KUELEKEA
siku ya wafanyakazi Mei Mosi, 2021 kituo cha Msaada wa Sheria kwa
wanawake (WLAC) wametoa wito kwa waajiri, Serikali na wadau mbalimbali
kuweka mifumo wezeshi na mazingira mazuri ya ajira ikiwemo kuweka sera
na kufanya mabadiliko ya kisheria zenye kuzingatia usawa wa kijinsia.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam leo Aprili 30, 2021
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Theodosia Muhulo amesema kuwa WLAC
kupitia Mradi wa uwezeshaji wa jamii kisheria juu ya sheria na haki za
ajira wamefanikiwa kutoa elimu kwa wanawake zaidi ya milioni nne.
Theodosia
amesema kuwa kupitia Mradi huo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu
wameweza kujitokeza kituo cha Msaada wa Sheria kwa wanawake (WLAC)
kudai haki zao.
Hata
hivyo Theodosia ametoa wito kwa wanawake kujitambua na kuwa na ujasiri
wa kupambani haki zao pale wanapoona haki zao zinayumbishwa.
Licha
ya hayo matokeo yaliyojitokeza katika Mradi unaofadhiliwa na Shirika
la Legal Serivices Facility waajiriwa wengi wameelimika baada ya
kuelimishwa na wamefanikiwa kufuata sheria na taratibu za ajira.
Amesema kuwa waajiri nao wameweza kuwapa mikataba ya ajirĂ , likizo na kuzingatia makato yaliyoainishwa kisheria wafanyakazi wao
Katika
kipindi cha Utekelezaji wa Mradi huo WLAC, imewafikia wafanyakazi 672
ambao kati yao wanawake ni 432 ambao wameweza kupata msaada wa kisheria
katika mashauri yao.
Naye
katibu wa chama cha wafanyakazi SBC, Bundi Clement, amesema WLAC
imekuwa mkombozi mkubwa katika kutoa elimu na ushauri kwa wafanyakazi
ambapo wengi wao wameweza kufaidika na kufurahia.
Kumekuwa
na elimu ya kutosha kutoka WLAC uliopelekea wafanyakazi kutambua hazi
zao kazini na pia elimu yao imepunguza migogoro mbali mbali ambapo awali
kabla hatujapata elimu ya kazi basi ilikuwa hata jambo dogo linaleta
usumbufu na kulifanya kubwa lakini sasa tumekuwa washauri wa mwajiri.
Kwa upande wake, Bhoke Makulu ambaye ni Mwalimu, ameishukuru WLAC kwa kusaidia wanawake wanaonyanyasika kazini.
Amesema
yeye alikuwa akifundisha shule binafsi lakini mkataba wake ulikatishwa
bila kufuata utaratibu lakini WLAC walimsikiliza.
"Kwa
kweli, hapa ni mahali ambapo nilikuwa na uwezo wa kujieleza na
kusikilizwa bila kukatishwa tamaa, ninatoa wito kwa kwa wanawake wote
mnaokutana na changamoto kazini na hata unyanyasaji wa namna zote
kufika WLAC kupata msaada." Amesema
Naye
katibu wa chama cha wafanyakazi SBC, Bundi Clement, amesema WLAC
imekuwa mkombozi mkubwa kwa wafanyakazi katika kutoa elimu na ushauri
kwa wafanyakazi ambapo wengi wao wameweza kufaidika na kufurahia.
Kumekuwa
na elimu ya kutosha kutoka WLAC uliopelekea wafanyakazi kutambua haki
zao kazini na pia elimu yao imepunguza migogoro mbali mbali ambapo awali
kabla hatujapata elimu ya kazi basi ilikuwa hata jambo dogo linaleta
usumbufu na kulifanya kubwa lakini sasa tumekuwa washauri wa mwajiri.
"Kadri
WLAC inavyozidi kuwasiliana nasi na kutoa elimu ndivyo na sisi
tunavyopata nafasi ya kutenda haki kwa wale tunaowaongoza." Amesema
Bundi.
No comments:
Post a Comment