Charles James, Michuzi TV
SIKU
moja baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mbunge na
Waziri wa Mambo ya
Balozi Mulamula ameyasema hayo leo nje ya Bunge alipokua akizingumza na Wandishi wa habari akiahidi pia kumsaidia Rais katika kukuza mahusiano ya Tanzania na Nchi zingine za nje.
Amesema hakuna shaka kwamba mahusiano ya Tanzania na Nchi zingine ni mapana sana ambapo anaamini yeye atakua msaada na mshauri mkuu wa Rais katika kukuza mahusiano ya kimataifa huku akibainisha kuwa Rais Samia nae ni Mtaalam wa mahusiano ya nje kuliko hata yeye.
" Rais Samia amekua mstari wa mbele katika kuendeleza na kukuza mahusiano mazuri na Nchi za kanda yetu ya Afrika Mashariki na Kanda ya SADC na mnaona jinsi ambavyo kama Nchi tulipata sapoti wakati wa aliyekua Rais Dk John Magufuli na alipoapishwa Mama Samia kuwa Rais wetu.
Kama mnavyojua mimi nilikua upande wa maziwa makuu kwa kipindi kirefu na ni kanda ambayo imekua na migogoro mingi lakini bado tumekua na mahusiano nayo mazuri, nachoamini nitaendelea kukuza na kuendeleza mahusiano mazuri na nchi zote ulimwenguni," Amesema Balozi Mulamula.
Amesema Tanzania kwa kipindi kirefu imekua na mahusiano mazuri na nchi zingine toka enzi za Baba wa Taifa licha ya kutokua na ubalozi kwenye kila nchi lakini bado tuna ushirikiano na haya mashirika ya kikanda jambo ambalo limekua likiimarisha mahusiano ya nchi yetu.
" Ninarudi nyumbani, ninarudi kwenye Wizara mama ni kama nilizaliwa kwenye wizara ya mambo ya nje nikakulia kwenye wizara ya mambo ya nje na sasa narudi tena ninaamini sitamuangusha Rais katika kukuza mahusiano yetu na Nchi zote duniani kwa faida yetu.
Kama mnavyojua Diplomasia yetu imekua Diplomasia ya Uchumi wanaita Economical Diplomacy sasa yote yaliyokua yakitendeka, Uwekezaji, Miradi mikubwa lazima tushirikiane na nchi zingine, na mashirika ya kifedha kukamilisha miradi yetu hii kwa maendeleo ya wananchi wetu," Amesema Balozi Mulamula.
Balozi Mulamula ameteuliwa jana na Rais Mama Samia kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akichukua nafasi ya Prof Palamagamba Kabudi ambaye amehamishiwa Wizara ya Katiba na Sheria.
No comments:
Post a Comment