Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kufungua Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani na Nje ya Nchi kilichopo Mbezi Luis Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Februari 2021.Viongozi wengine katika picha ni Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakar Kunenge, Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, Katibu Mwenezi wa CCM Humphrey Polepole wakishuhudia tukio hilo.
Taaswira ya Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani na Nje ya nchi kilichopo Mbezi Luis Jijini Dar es Salaam ambacho leo tarehe 24 Februari 2021 kimefunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. Kituo hiki kitakuwa na uwezo wa kuhudumia Mabasi 3,456 kwa siku, abiria 224,000 kwa siku, uwezo wa kuegesha magari madogo zaidi ya 280, Mabasi 1000 wakati wa usiku, Ofisi za Mabenki, Hoteli, Ofisi za Uhamiaji, Maduka pamoja na Ofisi mbalimbali- PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment