Pages

Wednesday, February 24, 2021

CHUO CHA TAIFA CHA UTALII (NCT) CHAASWA KUWAANDAA WANAFUNZI WATAKAO KWENDA KUJIAJIRI WAO WENYEWE NA KUTANGAZA BIDHAA YA UTALII KUPITIA ELIMU WALIYOIPATA CHUONI \

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akisisitiza kuhusu umuhimu wa  kuboresha elimu ya Wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) wakati wa kikao na Menejimenti ya  Chuo hicho kilichofanyika Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (katikati)  akieleza  umuhimu wa kutoa elimu ya masoko kwa wanafunzi wanaosoma katia Chuo chaTaifa cha Utalii kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Shogo Mlozi (kulia)   wakati wa  Kikao na Wajumbe wa  Menejimenti  kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaama

Naibu Wzairi wa Maliasili na Utalii, Mhe Mary Masanja (Katikati) akitoa maelekezo ya namna ya kuboresha vyumba vya malazi vinavyopatikakana  katika Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT)mara baada ya Kikao na uongozi wa Chuo hicho kilichofanyika leo  Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Shogo Mulozi.

…………………………………………………………………………………………..

Serikali imekitaka Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania kiendelee kusimamia taratibu na

miongozo ya ubora wa elimu iliyowekwa ili kuwajengea uwezo wanafunzi wanaohitimu chuoni hapo kujiajiri wenyewe na kuwa mabalozi wazuri wa kutangaza bidhaa  za  utalii zinazo patikana hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Utalii  Mhe. Mary Masanja alipokutana na Menejimenti ya Chuo hicho jijini Dar es Salaam.  Mhe. Masanja  amesema ni  muhimu Chuo hicho kinapofundisha wanafunzi kiangalie namna  ya kuwajengea uwezo wanafunzi hao kwenda kujitegemea pia  kiangalie namna ya kupata masoko kwa ajili ya kuwashawishi watalii wa ndani na nje ya nchi waje kutalii hapa nchini.

Mhe. Masanja  amesema pamoja na chuo hicho kutoa elimu ya masuala ya Utalii kinapaswa kufikiria namna ya kujitanua ili kiweze kuuza bidhaa  zake na kuongeza mapato kupita utalii kwa muda mfupi.
‘’ Mnapaswa kujitangaza kupitia huduma  mnazotoa, mnaweza kuona ni kituo kidogo lakini  mnaweza kujikuta mmefika mbali zaidi’’ amesisitiza Mhe. Mary

Katika  hatua nyingine Mhe. Mary ametoa wito kwa vijana wanaosoma masuala ya Utalii chuoni hapo waweke bidii katika kujifunza na  kuzifahamu lugha mbalimbali ili waweze kuwasiliana vizuri na kuwahudumia watalii wanaokuja hapa nchini.

 

No comments:

Post a Comment