Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza baada ya uzinduzi wa
usambazaji wa vitabu vya kiada vya darasa saba nchini leo Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipongezana na Mkurugenzi Mkuu wa
Taasisi ya Elimu Tanzania TET Dkt. Aneth Komba baada ya uzinduzi wa
usambazaji wa vitabu vya kiada vya darasa la saba nchini uliofanyika leo
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi
ya Elimu Tanzania TET Dkt. Aneth Komba (kulia) wakitazama baadhi ya
vitabu vitakavyosambazwa nchini
Washiriki wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa usambazaji wa vitabu vya kiada vya darasa la saba nchini leo Jijini Dar es Salaam.Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizindua
usambazaji wa vitabu vya kiada vya darasa la saba nchini leo Jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akipata picha ya pamoja na wadau
mbalimbali wa elimu nchini katika uzinduzi wa usambazaji wa vitabu vya
kiada vya darasa la saba nchini leo Jijini Dar es Salaam.
************************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Jumla ya nakala Milioni
4,443,586 za vitabu vya kiada Darasa la saba vimesambazwa nchini
ambavyo
vitagawiwa kwa uwiano wa kitabu kimoja wananfunzi wawili ikiwa lengo la
serikali kufikia uwiano wa kitabu kimoja kwa mwanafunzi mmoja.
Akizungumza baada ya uzinduzi
wa usambazaji vitabu hivyo leo Jijini Dar es Salaam,Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako,ameagiza kuanzishwa kwa
Vilabu vya historia na uzalendo katika shule za Msingi na Sekondari
nchini ili kujenga misingi ya kulinda tunu za taifa kwa wanafunzi.
Amesema hatua
hiyo ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli,
alilolitoa Desemba 9, mwaka jana alipoapisha Baraza la Mawaziri, ambapo
alitaka somo la historia kuwa la lazima na lijikite katika historia ya
nchini.
Profesa
Ndalichako alitoa agizo hilo jijini Dar es Salaam jana, wakati akizindua
usambazaji wa vitabu vya kiada vya Darasa la Saba na machapisho
mbalimbali.
Alisema kwa hatua
za mwanzo za utekelezaji wa agizo hilo Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),
iandae muongozo wa uanzishwaji wa vilabu hivyo katika shule zote nchini
na kutaka litekelezwe ndani ya mwezi huu.
Profesa
Ndalichako alisema hatua hiyo ni muhimu katika kujenga ujuzi na uelewa
mpana wa historia ya nchi kwa kizazi cha sasa, ambacho kinakabiliwa na
hombwe la ufahamu wa somo hilo.
“Katika hatua za
mwanzo tunaweza kuwajengea ujuzi huo hata kwa midahalo shuleni, TET itoe
muongozo wa namna ya kutengeneza klabu hizo na maudhui yake ili vijana
watambue historia yetu,” alisema.
Kwa mujibu wa
Profesa Ndalichako, utekelezaji wa hilo, uambatane na kuandaliwa kwa
maudhui na mtaala wa somo la historia litakalofundishwa shuleni.
Alisema ni budi
mtaala huo, uzingatie unoreshaji wa somo hilo kwa kujikita kwenye
historia ya nchini, kwani huo ndiyo msingi wa kujenga uzalendo wa nchi
kwa vijana.
“Naliagiza Baraza
lifuatilie utekelezaji wa Agizo la kuboresha somo la historia ili
lijilite katika kuwajengea Watoto uzalendo na mwishoni mwa Januari walau
maudhui zitambuliwe kwa ngazi ya msingi na sekindari ili kuanza
kufikiria kutengeneza mitaala,” alisema.
Aliagiza utekelezaji wa hilo uhusishe wadau
wataalamu wa historia kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali nchini na wazee ili
kuipata historia halisi ya taifa.
“Tunataka kila mtu aone ufahari kusoma
historia kwani itahusisha mambo ya Tanzania yake ukizingatia kwa sasa
nchi inasifika kwa mambo mengi, kama waasisi walilinda tunu za taifa
hatua budi kujenga vijana watakaoendeleza hilo, ” alisema.
Kuhusu vitabu vinavyosambazwa Profesa
Ndalichako alisema Serikali imegharimia sh. bilioni 6.4 katika kuviandaa
na kwamba jumla ya machapisho 5, 368, 362 vikiwemo vitabu 4, 443, 586
vya Darasa la Saba vimechapiahwa na vinasambazwa.
Alisema vitabu hivyo vinasambazwa na Jeshi
la Wananchi Tanzania (JWTZ) katika Halmashauri mbalimbali nchini, hivyo
ni jukumu la halmashauri hizo kuhakikisha zinavifikisha shuleni haraka.
Kulingana na Waziri huyo, hadi sasa kutokana
na vitabu vilivyopo wamefanikiwa kufikia uwiano wa kitabu kimoja kwa
wanafunzi wawili na mpango ni kufikia kitabu kimoja kwa mwanafunzi
mmoja.
Aliongeza kuwa ili kupunguza gharama za
uchapaji serikali imenunua Mashine kwa sh. bilioni sita, ambazo
zinatarajiwa kufungwa na kuanza kutumika mwezi huu.
Kadhalika, Profesa Ndalichako alisisitiza matumizi ya vitabu vyenye ithibati ili kuepuka makosa na upotoshaji kwa wanafunzi.
Alitaka vitabu kuacha kuwekwa makabatini kwa
kile kinachoelezwa kuwa ni utunzaji, badala yake vigawiwe kwa wanafunzi
ili vitumike ipasavyo.
Pia, aliagiza kumalizwa kwa changamoto ya
upatikanaji wa vitabu vya baadhi ya masomo ya sekondari kufikia mwezi
Machi mwaka huu.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET Dkt. Aneth Komba
amewataka walimu kuhakikisha kuwa wanatumia vitabu vinavyosambazwa na
taasisi hiyo ipasavyo ili kuweza kuwapatia wanafunzi haki yao ya msingi.
“Taasisi iliwahi
kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya vitabu na kubaini kuwa zipo baadhi ya
shule ambazo walimu hufungia vitabu kabatini kwa kuogopa kuwa
vitachakaa”. Alisema Dkt.Aneth.
Aidha Dkt.Aneth
alisema vilevile wanasambaza jumla ya nakala 253,408 za kiongozi cha
mwalimu darasa la saba, nakala 43,671 ya mtaala wa Elimu ya msingi
darasa la I-VII na nakala 305,697 ya mihtasari ya darasa la III-VII.
No comments:
Post a Comment