Amani Mayala, UDSM CBS
Katika
miaka ya hivi karibuni, mapinduzi ya teknolojia za kidijitali yamekuwa
mengi. Hii imezipa nchi nyingi faida bunifu za kupambana na changamoto
mbalimbali.Mfano wa faida hizo ni huduma za afya kwa njia ya mtandao
(m-health).
Kwa
watoa huduma za afya wengi, m-health imeleta njia mpya za namna ya
kutoa huduma ya afya kwa wahitaji. Kwa mujibu wa kampuni ya utafiti ya
Deloitte, m-health ina tija kwa wote, wagonjwa na watoa huduma kwa
wagonjwa. Mfano, mgonjwa anaweza kutumia mtandao kuperuzi dalili za
ugonjwa na kushirikisha wengine ili kupata tiba stahiki.
Jinsi
ambavyo ukuaji wa teknolojia na matumizi ya simu unaongezeka, idadi ya
watu wanaotumia na kufaidika na m-health nayo itaendelea kuongezeka.
Wataalamu wa sekta ya afya na teknolojia wanasema kwamba Tanzania iko
katika nafasi nzuri ya kufurahia matunda ya maendeleo haya ya
kiteknolojia katika sekta ya afya.
Mfano,
mgonjwa anayeweza kusoma vyema dalili za ugonjwa wake kwa njia ya
mtandao anaondoa ulazima wa kwenda hospitali kwa baadhi ya matatizo.
Katika eneo jingine, jumbe fupi za simu (SMS) zimesaidia kuwapa kina
mama wanaonyonyesha taarifa sahihi kuhusu lishe kwa watoto wao.
Wakati
tunafurahia teknolojia hizi na tija katika maisha yetu, ni vyema
kukumbuka mchango mkubwa wa kampuni za mawasiliano ya simu ambazo
zimetuwezesha kufikia maendeleo haya kwenye m-health. Mbali na kuweka
miundombinu sahihi ya huduma hizi kukua, kampuni za simu pia zimeendelea
kuwa bunifu kuwezesha wateja wake kupata huduma hizo.
Tigo
Tanzania, mmoja ya kampuni kubwa za mawasiliano ya simu za mkononi
nchini inawapa wateja wake, huduma hizi za m-health kama bima za afya na
maisha. Huduma kama hizi zinaonesha namna gani kampuni hizi
zinajiongeza na kwenda mbali zaidi kuhudumia wateja wake kwa ubunifu.
Tigo
pia imewezesha usajili wa vizazi kipitia njia ya mtandao na hivyo
kuwezesha upatikanaji wa haraka wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto. Hii ni
hatua muhimu kwani cheti cha kuzaliwa ni nyaraka muhimu na ya awali kwa
maisha ya binadamu yeyote ili kuweza kupata huduma zinazofuatia
maishani kama afya, fedha, na kadhalika.
Tukiendelea
kufurahia mchango huu wa kampuni za simu katika kuleta tija kwenye
maisha yetu, tuendelee kuzijengea mazingira bora ya kufanya kazi hapa
nchini Tanzania na kuziunga mkono ili ziendelee kufanya kazi bora zaidi.
No comments:
Post a Comment