Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Dodoma,Sosthenes Kibwengo,akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dodoma jinsi walivyofanikisha kufakisha
mahakama ya Hakimu Mkazi watu wanne pamoja na kurejesha Serikali zaidi
ya sh.11 ambazo alilipwa Marehemu
…………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kurejesha Serikalini zaidi
ya shilingi milioni 11 ambazo zililipwa kwenye akaunti ya benki ya
mtumishi marehemu kama mshahara kuanzia Oktoba 13, 2013 hadi Machi 2016
kinyume cha utaratibu.
Aidha TAKUKURU imewafikisha
mahakama ya Hakimu Mkazi watu wanne na kuwafungulia mashauri mawili
yenye jumla ya mashtaka 28 yanayohusu vitendo vya rushwa na kugushi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mkuu wa Takukuru mkoani Dodoma Sosthenes Kibwengo,wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Kibwengo amesema kuwa
shauri la kwanza la jinai linamkabili Aithan Chaula (61) aliyekuwa
Afisa Kilimo wa halmashauri ya Chamwino na mratibu wa pembejeo za kilimo
za ruzuku kwa msimu wa 2015/16 na Michael Mpembwa (44) ambaye ni
Mkurugenzi wa kampuni ya Agro Suppy iliopewa uwakala wa kusambaza
pembejeo za kilimo katika kijiji cha Zajilwa kilichopo wilayani humo
jijini hapa.
Amesema kuwa watuhimiwa hao watashtakiwa kwa makosa 25 ya kughushi kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16.
Kibwengo amesema
kuwa uchunguzi unaonyesha kuwa kati ya Januari na Agosti 2016
watuhumiwa hao waligushi nyaraka ambazo zilionyesha kwamba wakala
alisambaza pembejeo zikiwemo mbegu za mahindi na mbolea kwa wakulima wa
Zajilwa na hivyo kulipwa sh miloni 14 wakati wakifahamu kwamba ni uongo.
Amesema kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007 na sheria nyinginezo.
Kibwengo ametaja
shauri la pili linamkabili Benedict Mazengo (58) aliyekuwa mtendaji wa
Kata ya Ntyuka na Jonathan Mwaluko (48) aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa wa
Chimala jijini hapa ambao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya ubadhilifu
kinyume na kifungu cha 28 (1) cha sheria ya kupambana na rushwa,matumizi
ya nyaraka kumdanganya mwajiri kinyume na kifungu cha 22 vyote vya
sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007 pamoja na kugushi
kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu Sura ya16.
Amesema kuwa
uchunguzi wa Takukuru unaonyesha kuwa Juni 2015 watuhumiwa waligushi na
kutumia nyaraka za maelezo ya uongo zilizowawezesha kutoa benki sh
milion 2.9 ambazo walizitumia kwa ubadhilifu badala ya kazi iliopangwa.
Aidha Kibwengo
amewasihi watumishi wa umma pamoja na wananchi kutambua kuwa rushwa ni
kosa la jinai na jinai huwa haifi,hivyo wahakikishe wanakwenda kulingana
na sheria,kanuni na taratibu za nchi.
No comments:
Post a Comment