Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe.
Angellah Kairuki, akisikiliza maelezo ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, kuhusu
mifumo ya fedha, sekta ndogo ya fedha na madeni, pensheni na bajeti,
alipotembelea katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika
Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya
Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe.
Angellah Kairuki, (kulia) akisoma chapisho la Bajeti ya Wananchi
alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya
Nanenane Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe.
Angellah Kairuki (kushoto), akitoa maelekezo kwa watumishi wa Wizara ya
Fedha na Mipango na Taasisi zake, alipotembelea katika Banda la Wizara
ya Fedha na Mipango, wa pili kushoto ni Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet
Hasunga na wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Mamlaka ya Udhibiti wa
Manunuzi ya Umma (PPRA) Bw. Mcharo Mrutu (kulia) akielezea mchakato wa
Zabuni za Umma wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto),
alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya
Nanenane Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu, katikati ni
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga.
Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano wa Taasisi ya UTT- AMIS, Bi.
Martha Mashiku, akifafanua jambo kuhusu masuala ya uwekezaji wa masoko
ya fedha, mitaji na dhamana za Serikali, wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki
(kushoto), alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika
Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi
Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe.
Angellah Kairuki (kulia) akizungumza jambo na watumishi wa Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM) alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na
Mipango, katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa, viwanja vya
Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe.
Angellah Kairuki (katikati), Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga,
wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha
na Mipango baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango,
katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa, viwanja vya
Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah
Kairuki, akizungumza jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, baada ya
kutembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya
Nanenane yanayofanyika Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
(Picha na Peter Haule, WFM)
*******************************
Na. Peter Haule na Farida Ramadhani, WFM, Simiyu
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki
amehimiza kutumia lugha rahisi na mitandao ya kijamii kufikisha taarifa
za masuala ya
uchumi na fedha kwa wananchi.
Rai hiyo ameitoa
alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya
Nanenane Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi, Mkoani
Simiyu.
Mhe. Kairuki
alisema kuwa ni vema Kampuni za simu za mikononi, tovuti na mitandao
mingine ya kijamii ikatumika kupeleka toleo la Bajeti ya Wananchi
kulingana na mahitaji husika ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Pia ameitaka
Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kusimamia taasisi za umma
kuhakikisha zinatoa fursa kwa makundi maalum kushiriki katika zabuni za
umma kama ambavyo sheria ya ununuzi wa umma inavyoeleza.
Mamlaka ya Masoko
ya Mitaji na Dhamana wametakiwa kuongeza kampuni zilizo jiorodhesha
kwenye Soko la Hisa kutoka kampuni 27 ili idadi hiyo ilingane na idadi
ya kampuni zilizosajiliwa kwenye Wakala wa Usajili wa Biashara na
Leseni-BRELA, zinazofikia zaidi ya elfu nane ili sekta ya masoko ya
mitaji na dhamana yawe chachu ya kukuza uchumi wa nchi.
Ameipongeza
Wizara ya Fedha na Mipango kwa kazi nzuri ya kuandaa mipango ya kitaifa
na usimamizi wa Sera za Bajeti na Fedha na kuwataka wataalam wa Wizara
hiyo kuongeza juhudi zaidi ili kuiwezesha nchi kufanikisha malengo yake
ya kuwahudumia wananchi wake.
Akimwongoza
kutembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Viwanja vya
Nyakabindi, Bariadi, mkoani Simiyu, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini wa Wizara hiyo, Bw. Benny Mwaipaja, alimweleza Waziri
Mheshimiwa Angellah Kairuki, kwamba Wizara ya Fedha na Mipango inatambua
mchango mkubwa unaotolewa na Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika
kukuza pato la Taifa.
Aidha alisema
kuwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, imefuta kodi zenye
kero zipatazo 105 katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kuongeza
tija kwa wakulima na kuwawezesha kuzalisha mazao kwa wingi.
Aidha alisema
kupitia taasisi zake za Wizara imetoa mchango mkubwa katika kukuza
masuala ya ushirika na mikopo kwa wananchi ambapo amesema Taasisi yake
ya Self Microfinance pekee, imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 36.3 kwa
vikundi vya wajasiliamali nchini kote.
Bw. Mwaipaja
alibainisha kuwa taasisi za elimu ya juu zilizopo chini ya Wizara ya
Fedha na Mipango kikiwemo Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Taasisi
ya Uhasibu Tanzania (TIA) zimetoa mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa
tafiti zinazofanywa na vyuo hivyo zinakidhi mahitaji ya kuisaidia jamii
hususani katika kuandaa maandiko ya miradi pamoja na huduma za ushauri.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mheshimiwa Angellah
Kairuki, alikuwa amemwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa, kwenye siku ya Ushirika,
wakati wa Maonesho ya siku ya Wakulima Nanenane katika viwanja vya
Nyakabindi mkoani Simiyu.
No comments:
Post a Comment