Pages

Monday, August 3, 2020

Benki ya CRDB kufungua tawi ndani ya Ukuta wa Magufuli, Mirerani, kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo


 Meneja wa Benki ya CRDB, Kanda ya Kaskazini Chiku Issa (Kushoto) akiwa na Mchimbaji madini Bilionea, Saninio Laizer (wa pili Kushoto), Meneja wa Biashara wa Kanda (CRDB), David Peter (Mwenye Miwani) na Meneja wa tawi la Mirerani kwa benki hiyo, David Ndohele.  (Picha na Pamela Mollel).
 Meneja wa Benki ya CRDB Chiku Issa akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la machimbo ya madini ya Tanzanite Mirerani (Picha na Pamela Mollel).
 Meneja wa Benki ya CRDB, Kanda ya Kaskazini Chiku Issa (wa tatu kulia) akimpongeza  Mchimbaji madini Bilionea, Saninio Laizer (Kushoto).
 Picha ya pamoja

Na Pamela Mollel, Mirerani
Benki ya CRDB imeanza mkakati wa kujenga tawi lake jingine na la kwanza katika eneo la uchimbaji madini la Mirerani, hususani ndani ya ukuta mkuu wa Magufuli.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Chiku Issa amesema taaasisi hiyo ya fedha ina madhumuni ya kupeleka huduma za kibenki karibu kabisa na wachimbaji wote wadogo kwa wakubwa wa eneo la Mirerani, maarufu kwa machimbo ya madini ya vito aina ya Tanzanite.
“Pia kuhakikisha kuwa miamala ya ununuzi na uuzaji inafanyika ki usahihi na kwa wakati, na vile vile kuwezesha ulipwaji wa kodi za serikali,” alisema Chiku ambaye aliongeza kuwa yeye binafsi amefika Mirerani kujifunza namna ya uchimbaji na uuzaji wa madini unavyoendeshwa ili aweze kuwasaidia wahusika.
Kwa mujibu wa meneja huyo, benki yake pia itawasaidia wachimbaji katika kuwapatia mikopo mbalimbali kuwasaidia katika mitaji na ununuzi wa vifaa vya shughuli zao kama mashine za kuchimbia na kuhudumia migodi yao.
Chiku ameeleza pia wanatoa pia ushauri kwa wachimbaji, akiwemo bilionea mpya Saninio Laizer, wa jinsi ya kuwekeza pesa zake kwa ajili ya kupata faida Zaidi. “Yeye ni mteja wetu mkubwa!” alisema.

No comments:

Post a Comment