Pages

Monday, August 31, 2020

TDL Yajizatiti kukuza sekta ya kilimo cha zabibu nchini


Mkulima wa zabibu Daniel Ngoima wa Kijiji cha Matumbulu nje ya Jiji la Dodoma  akivuna zao hilo kama alivyokutwa  shambani kwake
Mkulima wa zabibu Victoria Zablon wa kijiji cha Matumbulu nje ya Jiji la Dodoma akionja sukari ya zao hilo
Baadhi ya wakulima wa zao la zabibu Kijiji cha Matumbulu nje ya Jiji la Dodoma wakiwa na makreti yenye zao hilo baada ya kuvuna tayari kwa kusafirishwa kupelekwa kiwandani kwa ajili ya uzalishaji wa vinywaji 
…………………………………………..
Kampuni  ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), imeeleza dhamira yake ya kuendeleza kilimo cha zabibu mkoani Dodoma pamoja na matarajio yake ya kuingia mikataba ya
kununua zabibu moja kwa moja kutoka kwa wakulima wadogo.
Mchango wa TDL wa sera yake ya kununua malighafi nchini  na dhamira ya kukuza sekta ya kilimo cha zabibu inaenda sambamba na jitihada za  serikali za kuboresha maisha ya wakulima wadogo na kukuza uchumi wa Tanzania.
TDL inaamini jitihada za Serikali za kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda zinaweza kufanikiwa  ikiwa wakulima wadogo wanawezeshwa kuzalisha malighafi inayohitajiwa na viwanda.
Meneja Mkuu wa TDL, Devis Deogratius, alisema kampuni hiyo kwa sasa inanunua takribani lita milioni 1.2 za mchuzi wa zabibu kwa mwaka kutoka kampuni za CETAWICO na UWAZAMAM, ambazo zinanunua zabibu za wakulima wa ndani  ambapo  inatumia bilioni 3.3 kwa mwaka.
Deogratius aliongeza kusema kuwa imedhamiria kununua malighafi ya ndani katika kipindi chote cha miaka ijayo ambapo kwa sasa inatumia malighafi na huduma za kufanikisha uzalishaji kwa asilimia 80% ambayo ni sasa na shilingi bilioni 46.
TDL imewekeza katika uundaji wa chapa za Kitanzania ambazo ni pamoja na: Imagi, Valeur, Wines Dodoma, Dodoma Rose, Konyagi na Zanzi Cream liqueur ambazo  zimetengenezwa kwa viwango vya ubora kwa  kimataifa kwa kulenga mahitaji ya makundi mbalimbali katika soko.

No comments:

Post a Comment