Mwalimu mkuu wa shule
ya awali na msingi New Light ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara, Tumaini Mbise akizungumza kwenye kikao cha
wazazi, walezi, wanafunzi na walimu wa shule hiyo.
Wanafunzi wa shule ya
awali na msingi New Light ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro
Mkoani Manyara, wakiwa kwenye kikao cha wazazi, walezi na walimu wao.
…………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu, Mirerani
JAMII imetakiwa
kutambua kuwa wasomi wanapaswa kuandaliwa ili baadaye wawe na faida
kutokana na elimu waliyonayo kwa watanzania wanaowazunguka na siyo
kuelimika kisha kutokuwa na msaada.
Mwalimu mkuu wa shule
ya awali na msingi New Light ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara, Tumaini Mbise aliyasema hayo juzi kwenye kikao
cha wazazi, walezi, walimu na wanafunzi wa shule hiyo.
Mwalimu Mbise alisema
elimu inapaswa kuwa inalenga matatuzi na siyo kuwa na maarifa mengi
yasiyo na ufumbuzi kwa jamii inayowazunguka.
Alisema kutokana na
hilo walimu wa shule hiyo ya New Light wanawajenga misingi bora
wanafunzi wao waweze kuwa jamii bora kuanzia sasa na miaka ijayo.
“Watu hawatakiwi kuwa
na mashaka na mtu mwenye elimu kwa kufanya mambo chanya kwani wasomi
wanapaswa kuandaliwa ili baadaye wawe na faida kutokana na elimu
waliyonayo,” alisema Mbise.
Alisema elimu
inapaswa kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha inayozunguka hivyo
wanafunzi wao wanawaandaa tangu wakiwa wadogo wakishirikiana na wazazi.
Katibu wa bodi ya
shule hiyo, Oscar Gunewe alisema shule hiyo inafungwa kwa muda wa wiki
moja ili kutoa nafasi ya likizo fupi kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Gunewe alisema
japokuwa kwenye muhula huu kulitokea janga la corona, lakini walimu
wametumia muda wa ziada kufidia masomo waliyokosa wanafunzi hao.
Mwenyekiti wa kamati
ya wazazi wa shule hiyo, George Martin aliwataka wazazi na walezi walipe
ada kwa wakati ili fedha hizo ziweze kutumika kwenye matumizi
mbalimbali.
“Kutokana ada
mnazozitoa ndiyo mishahara ya walimu inapatikana hapo na kama huna fedha
zote muwe mnalipa kidogo kidogo hadi mmalize,” alisema.
No comments:
Post a Comment