*********************************
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza
Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora kwa kazi nzuri inayofanywa na
Tume hiyo kwa kuweza kutatuwa Changamoto mbalimbali za Wananchi na
kuweza kupata Haki zao pale wanapozulumiwa.
Makamu wa Rais
amesema hayo leo alipokutana na Ujumbe wa Makamishna wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora uliyoongozwa na Mwenyekiti wa Tume Hiyo Jaji
Mstaafu Mathew Mwaimu walipomtembelea kwenye Makazi yake Kilimani Jijini
Dodoma.
Aidha Makamu wa
Rais ameipongeza Tume hiyo kwa kuweza kubadilika na kufanya kazi vizuri
pamoja na kutenda Haki kwa Wananchi na Taasisi zote kwa ujumla.
Nae Mwenyekiti wa
Tume ya haki za Binaadamu na Utawala Bora Jaji Msaafu Mathew Mwaimu
ameipongeza Serikali kwa kuweza kuwaletea Wananchi maendeleo Bora na
kuitakia kila la heri katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Jaji Mwaimu
amesema kuwa Tume yake haipendezewi na vitendo vya baadhi ya Viongozi wa
Vyama vya Siasa ambao wamekuwa wakisema Watu baada ya kunadi Sera za
Vyama vyao.
No comments:
Post a Comment