Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (kushoto) akiwa na Mtendaji Mkuu
wa TAHA Dkt.Jacqueline Mkindi (kulia) mara alipokabidhi ramani ya
Tanzania inayoonyesha maeneo yaliyopimwa afya ya udongo kwa matumizi ya
wakulima nchini.Hafla hiyo imefanyika jijini Arusha leo
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (kushoto) akikabidhi ramani
inayoonesha maeneo yaliyopimwa afya ya udongo kwa Mtendaji Mkuu wa TAHA
Dkt.Jacqueline Mkindi leo walipofanya mazungumzo jijini Arusha kuhusu
uendelezaji wa tasni ya mboga mboga na matunda.(horticulture).
(Picha na habari na Wizara ya Kilimo)
******************************************
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw.
Gerald Kusaya amefanya kikao na Mtendaji Mkuu wa
Taasisi ya Kuendeleza Mazao ya Bustani (TAHA) Dkt.Jacquline Mkindi
jijini Arusha cha
kujadili mikakati na mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya tasnia ya mboga mboga na matunda (horticulture) nchini.
Sambamba na kikao hicho,
Katibu Mkuu Kusaya ameikabidhi TAHA zawadi ya Ramani ya Tanzania
inayoonesha viwango vya pH na Afya ya Udongo kwa nchi nzima na
imepokelewa na Mtendaji Mkuu wa TAHA, Dr. Jacqueline Mkindi.
Kusaya ameitaka TAHA kuendelea
kuelimisha wakulima wengi zaidi kuzingatia kilimo cha kitaalam kwa
kutambua aina ya udongo unaofaa kwa zao husika na mbolea gani itumike,
ndio maana amekabidhi ramani hiyo kuwezesha utambuzi wa maeneo yanayofaa
kwa mazao ya horticulture nchini.
“Tunaendelea kuishukuru
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano mkubwa na wa muda wote
inaotupatia wadau wa sekta ya horticulture ” Dr Mkindi alisema.
Katibu Mkuu Kusaya alikuwa mkoani
Arusha Kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kutembelea taasisi
zinazojihusisha na kilimo vikiwemo viwanda vya kuzalisha mbolea kwa
matumizi ya kilimo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment