Mtaalamu wa Huduma Ndogo za Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,
Bi. Janeth Hiza (kushoto), akitoa elimu ya Sheria ya huduma hiyo kwa
wanawake kutoka Bariadi Mkoani Simiyu walio katika vikundi mbalimbali
vya VICOBA, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika
Maonesho ya Nanenane Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Wakazi wa Mkoa wa Simiyu Bi. Mwinza Maghembe na Mbula Mayenga, wakipewa
elimu ya huduma ndogo za fedha kutoka kwa Mtaalamu wa Sekta hiyo wa
Wizara ya Fedha na Mipango. Bi. Limi Burugu (kushoto), walipotembelea
Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa,
viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Wakazi wa Bariadi Mkoa wa Simiyu (kushoto) wakipewa maelezo juu ya
mifumo ya malipo ya Serikali kutoka kwa mtaalamu wa mifumo hiyo wa
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Chilumba, walipotembelea Banda
la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa,
viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Mtaalamu wa Sheria kutoka Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), Bw. Amosi
Manyama (kulia), akitoa maelezo kuhusu utaratibu wa kujiunga na Chuo
hicho na Kozi zinazopatikana kwa wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu,
walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya
Nanenane Kitaifa viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Bi.Mwinza Maghembe na Mbula Mayenga (kulia), wakazi wa Bariadi Mkoani
Simiyu, wakielekezwa jambo na Afisa Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya
Fedha na Mipango, Bi. Farida Ramadhani, walipotembelea Banda la Wizara
ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika viwanja
vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi
Serikalini (GPSA) Bw. Peter Mayila, akisikiliza kwa makini maswali ya
Bw. Benedicto Wilison, kuhusu majukumu ya Wakala huo, alipotembelea
Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa
viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.Muonekano wa Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa, viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu
(Picha na Peter Haule, WFM)
No comments:
Post a Comment