Pages

Thursday, July 2, 2020

TANZANIA YAVUNJA REKODI YA KUINGIA UCHUMI WA KATI KABLA YA LENGO LA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO



Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akitangaza siri 10 za Tanzania kung’ara na kuingia Uchumi wa kati miaka mitano kabla ya kabla ya lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi,akifafanua jambo zaidi kwa waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akitangaza siri 10 za Tanzania kung’ara na kuingia Uchumi wa kati miaka mitano kabla ya kabla ya lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025.
………………………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
Tanzania yavunja rekodi kwa kuingia kwenye uchumi wa kati  miaka mitano kabla ya lengo la
Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 jambo ambalo linaifanya Tanzania kuandika historia dunia.
Kauli hiyo inatokana na Benki ya Dunia kuitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 50 duniani za uchumi wa kipato cha kati, ikiwa ni ya pili baada ya Kenya katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, baada ya ukuaji wa uchumi unaosukuma pato la mwananchi kukua (Per capita GNI) mwaka 2020. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma,  amesema kuwa  kwa mujibu wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2025 katika ukurasa wa pili, kipengele 1.2 Uchumi wa kipato cha kati umehusishwa na kuwa na nchi ambayo umaskini unapungua, uchumi imara unaojengwa na kuimarika kwa uzalishaji viwandani unaimarika na wananchi wanapata maendeleo.
Dkt. Abbasi ameeleza kuwa uchumi wa kipato cha kati umegawanyika katika madaraja mawili daraja la chini ambapo ni kuanzia dola za Kimarekani 1036 hadi 4045 na daraja la juu ni  dola 4046 hadi 12,535 na mwaka huu Tanzania imepanda daraja kuwa uchumi wa kipato cha kati daraja la chini, pamoja na nchi za Algeria na Benin.
Pia Dkt. Abbasi amebainisha siri 10 zilizoisaidia Tanzania kutajwa kufikia daraja la uchumi wa kipato cha kati na  Benki ya Dunia hapo Julai 1, 2020 kuwa ni nchi yenye amani na utulivu, na hivyo ni msingi muhimu nyuma ya mafanikio  ya nchi ya Tanzania  kuingia katika uchumi wa kipato cha kati kwani  bila amani hakuna kufanyakazi, hakuna kuzalisha na hakuna kuongeza kipato.
“hivyo viongozi, wanahabari  na wananchi kwa ujumla  niwasisitizwa  kuwekeza akili zao katika kuimarisha amani iliyopo na kukataa chokochoko zozote zile zinazoweza kuharibu misingi ya maendeleo”ametoa wito Dkt. Abbas.
Aidha Dkt. Abbasi amesema siri nyingine  ni utekelezaji usioyumba, katika miaka 59 ya Uhuru na mitano ya Awamu ya Tano Serikali imejitahidi kusimamia eneo hilo kwa  kuhakikisha mipango inayowekwa inatekelezwa kwa kina (3feet implementation).
 Dkt. Abbasi  amesema kuwa azma ya kujitegemea, nidhamu katika matumizi, kutekeleza miiko ya uongozi, kuwekeza kwenye miradi inayochemsha uchumi, maendeleo ya vitu na sekta binafsi yenye tija ndio chachu ya Tanzania kufikia hapa ilipo leo.

No comments:

Post a Comment