………………………………………………………………………….
Na John Walter-Babati
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoani Manyara imefanikiwa kurejesha zaidi ya shilingi milioni nne za watumishi wa shule ya msingi Birsima, ambazo
zilifanyiwa ubadhirifu na Mwalimu
mkuu msaidizi wa shule hiyo, Aman Paul Mkeni.Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoani Manyara imefanikiwa kurejesha zaidi ya shilingi milioni nne za watumishi wa shule ya msingi Birsima, ambazo
Taarifa iliyotolewa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Holle Makungu imesema Fedha hizo zimekabidhiwa kwa wahusika na afisa wa TAKUKURU dawati la Udhibiti Bi.Edda Senkondo leo juni 30,2020.
Kwa mujibu wa mkuu wa TAKUKURU Manyara Holle Makungu, amesema Mkeni ambaye pia ni Mhasibu wa shule hiyo iliopo wilayani Babati, alishindwa kutimiza wajibu wake wa kuwalipa fedha hizo watumishi hao wasio walimu na kuzifanyia ubadhirifu.
Watumishi Waliokabidhiwa fedha zao kwenye mabano ni Ezekiel Rory (410,000), Daniel Jacob (1,400,000) na Melania Bayo (300,000).
Amesema wamefanikiwa kurejesha fedha hizo baada ya kupata malalamiko ndipo walipomtaka Mwalimu Mkeni kuwasilisha fedha hizo.
Hata hivyo Makungu ameshauri uongozi wa shule hiyo umpe mwalimu mwingine mwenye uadilifu kazi ya kutunza fedha kwa kuwa Mwalimu huyo hastahili.
No comments:
Post a Comment