Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akipokea maelezo kutoka kwa
Mkuu wa wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, Mhe. Benson Kilagi mara baada
ya kufika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya leo tarehe 31 Julai, 2020.
Katibu
Mkuu Kilimo Bwana Gerald Kusaya akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Itilima, Mhe. Benson Kilangi pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikandilo
mwenye fulana nyekundu pamoja na Wakulima na Wananchi baada ya Katibu
Mkuu kukagua mipaka ya eneo lililotolewa na Wananchi hao kwa ajili ya
ujenzi huo, mapema leo, tarehe 31 Julai, 2020.
Katibu
Mkuu Kilimo Bwana Gerald Kusaya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Bibi. Elizabeth Gumbo pamoja na
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikandilo, mwenye fulana nyekundu pamoja na
Wakulima na Wananchi baada ya Katibu Mkuu kukagua mipaka ya eneo
lililotolewa kwa ajili ya ujenzi huo, mapema leo, tarehe 31 Julai, 2020.
Katibu
Mkuu Kilimo Bwana Gerald Kusaya akifuatilia maelezo kutoka kwa Mkuu wa
wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi alipokuwa akizungumza na Wakulima
wa kijiji cha Ikindilo ambapo kwa kauli moja, wameridhia na kutoa eneo
ambalo litajengwa ghala la kuhifadhia mazao ya kilimo.
Katibu
Mkuu Kilimo Bwana Gerald Kusaya akipokea taarifa ya maendelo ya Sekta
ya Kilimo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Itilima, Bibi Elizabeth Gumbo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya mara baada ya kufika kwenye
Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima leo tarehe 31
Julai, 2020.
***********************************
Serikali ya Rais, Dkt. John Pombe
Magufuli imetoa kiasi cha Dola za
Marekani milioni 35.3 sawa na bilioni
78 fedha Kitanzania kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Kudhibiti
Sumukuvu nchini (Tanzania Prevention for Afflatoxin Contamination –
TANPAC).
Sumukuvu inatokana na fangasi
wanaoota kwenye mazao ya chakula hususan mahindi na karanga, ambapo
fedha hizo zitatumika kujenga miundombinu mbalimbali, ikiwemo maghala
katika Halmashauri 14 Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza kabla ya kutembelea
eneo litakalojengwa ghala la kuhifadhia mazao ya chakula katika kijijini
cha Ikindilo wilayani Itilima mkoani Simiyu, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo, Bwana Gerald Kusaya anasema fedha hizo zitatumika kujenga
maabara mahususi ya kilimo Jijini, Dodoma; Kituo cha karantini ya
utafiti wa Sumukuvu, Kibaha mkoani Pwani pamoja na Kituo mahili cha
mazao eneo la Mtanana, mkoani Dodoma.
Aidha, Katibu Mkuu Kusaya amesema
kupitia mradi wa TANPAC Serikali itajenga Maghala 14 kwa ajili ya
kuhifadhi mazao ya chakula aina ya nafaka na kutumia fursa hiyo kuziomba
Halmashauri hizo 12 (Tanzania Bara) na mbili Zanzibar kutoa maeneo
ambayo hayatakuwa na migogoro ya ardhi ili maghala hayo yajengwe mara
moja.
Katibu Mkuu Kusaya ameongeza kuwa
thamani ya kila ghala, litakalojengwa katika Halmashuri kila
Halmashauri; Litagharimu kiasi cha shilingi milioni 480 na kuongeza kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kumkomboa Mkulima kutokana na
changamoto ya sumukuvu ambayo ina athari kubwa kwa afya za walaji pamoja
na biashara ya mazao ya kilimo ndani na nje ya nchi.
“Nawaomba Wakurugenzi wa
Halmashauri, Wakuu wa Wilaya, Wakulima na Wananchi ambao Halmashauri zao
zimepata fursa ya kujengewa maghala haya, waridhie na wataoe maeneo
ambayo hayana migogoro ili mwezi Disemba, 2020 tuanze ujenzi, fedha ipo
tayari na mchakato wa kuwapata Wazabuni upo kwenye hatua ya mwisho.”
Amekaririwa Katibu Mkuu Kilimo, Bwana Gerald Kusaya.
No comments:
Post a Comment