SHEIKH
Ahmed Ashkina askisoma Hutba ya Sala ya Eid Alhajj baada ya kumalizika
kwa Sala hiyo iliofanyika Kitaifa Mkoa wa Kaskazini Unguja Wilaya ya
Kaskazini “B”,katika uwanja wa mpira wa Misuka Mahonda.(Picha na Ikulu) MASHEIKH
wa Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja wakimsikilia Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Alhajj Dk. Ali Mohamed
Shein.(hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” Kinduni.(Picha na Ikulu) RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali
Mohamed Shein, akizungumza na Masheikh wa Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja
katika ukumbi wa Halmashauri Wilaya Kinduni, baada ya kumaliza Sala ya
Eid Alhajj iliofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Misuka Mahonda.(Picha
na Ikulu) RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Alhajj Dk. Ali
Mohamed Shein, akimsalimia Mtoto Ali Abdalla Hassan, baada ya
kumalizikac kwa Sala ya Eid Alhajj iliofanyika Kitaifa katika Uwanja wa
Mpifra wa Misuka Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja leo
31-7-2020.(Picha na Ikulu) RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhajj Dk. Ali
Mohamed Shein, akiitikia dua ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar
Sheik. Hassan Othman Ngwali (hayupo pichani) na (kushoto kwa Rais) Mufti
Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi, Spika wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utawala Bora na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali Suleiman na (kulia
kwa Rais)Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe. Khamis Juma Mwalim na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi,
wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla ya Sala ya Eid Alhajj
iliofanyika Kitaifa Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja katika Uwanja wa
mpira wa Misuka mahonda.(Picha na Ikulu)WAUMINI
wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa Sala
ya Eid Alhajj iliofanyika Kitaifa Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja katika
Uwanja wa Mpira Mahonda.(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment