Afisa Ushirika wa wilaya ya Nyasa Bw.Menance Ndomba Akifungua mmafunzo
ya wakulima wa Chama cha Ushirika cha msingi na Mazao na Masoko cha
Kingerikiti AMCOS yaliyofanyika hivi karibuni Kingerikiti Wilayani
Nyasa. Mkufunzi
wa mafunzo kutoka Shirika la Sturbucks Bi Bahati Mlwilo akifundisha
wakulima wa kata ya Kingerikiti ili kuwawajengea uwezo wa kulima wa
kahawa kulima kitaalamu na kufikisha katika soko kahawa yenye ubora.
***********************************
Chama cha cha Ushirika cha Msingi
cha Mazao na Masoko cha Kingerikiti (Amcos), kwa
kushirikiana na
Wafadhili wa chama hicho kutoka Nchini Marekani kupitia Shirika la
USADF, Hivi karibuni Kimetoa Mafunzo kwa wakulima wa kahawa, yenye
lengo la kuwajengea uwezo wa kuzalisha na kuandaa kahawa bora ili
kuongeza kipato kwa Mkulima.
Mafunzo hayo ya siku mbili,
yametolewa katika Ofisi za Chama, zilizopo Katika Kijiji cha Kingerkiti,
Kata ya Kingerikiti Wilaya ya Nyasa, na yametolewa na wakufunzi kutoka
Shirika la Sturbucks yenye lengo la kuwafundisha wakulima namna ya
kulima, kuitunza na kuandaa kahawa yenye Ubora ili kuifikisha Sokoni.
Akifungua Mafunzo hayo Afisa
Ushirika wa Wilaya ya Nyasa Bw.Menance Ndomba alikipongeza chama hicho
kwa kutoa mafunzo kwa wakulima yatakayowawezesha Wakulima, kukabiliana
na wadudu waharibifu wa zao la kahawa ambalo pia ni zao la Kimkakati.
Aidha ametoa Wito kwa wanaushirika
kushikamana, ili kuuendeleza Ushirika kwa kuwa ndiyo nguzo pekee kwa
Wakulima wa Zao la Kahawa ambayo huwawezesha kuunganisha nguvu zao
wakati wakuyafikisha mazao yao sokoni na kuhakikisha chama kinakwenda
vizuri kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana hivyo wana kila sababu ya
kushikamana.
“Ndugu zangu wanaushirika wa Chama
Cha Msingi cha Mazao cha Kingerikiti, Nichukue Fursa hii kuwapongeza
Viongozi wa Chama na wafadhili wa Chama hiki, USADF kwa kutoa mafunzo
ambayo yanawajengea uwezo wakulima namna ya kulima, kupambana na wadudu
waharibifu na kuiandaa kahawa bora itakayo washawishi wanunuzi, wanunue
kahawa iliyokuwa na viwango vinavyokubalika na kwa bei nzuri, Aidha
napenda kuwafahamisha rasmi kwamba kufuatia mafunzo haya mmeanzisha
rasmi mchakato wakuyafikia masoko maalumu na kwa sasa tunajisajiri SOKO
la CAFÉ Practice Nasema ahsante sana, Nitoe Wito kwa wanachama wa Chama
hiki kushirikiana na kuendeleza Ushirika huu kwa kuwa Vyama vingi
vikishapata mafanikio basi kutoelewana kunaanza kwa lengo la kuvuruga
Ushirika, ” Alisema Ndomba.
Bw Ndomba aliyataja mafanikio
yaliyopatikana Kingerikiti Amcos ni pamoja na kuwa na Mfuko wa Pembejeo
wenye thamani ya milioni 38 ambao huwakopesha wakulima pembejeo na
kulipa kipindi cha mavuno hali iliyosababisha kuongezeka kwa uzalishaji
kutoka tani 10.3 mwaka 2017/2018 hadi kufikia tan 360.34 kwa Msimu wa
mwaka 2019/2020. Mafanikio mengine nikukarabati ofisi na kununua vifaa
vya ofisi, na kununua Mtambo wa kuchakata kahawa wenye thamani ya
miliono 47.
Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo
kutoka Shirika la Sturbucks Bi Bahati Mlwilo amesema mafunzo
yaliyotolewa kwa wakulima yamewajengea uwezo wa kulima kahawa ya Kisasa,
kupambana na Wadudu wanaoharibu kahawa, namna ya kupambana na magonjwa
ya kahawa.lakini pia wamejifunza namna ya kuiandaa na kuifiiksha kahawa
yenye ubora na kuongeza kipato kwa kaya na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wao Washiriki wa
mafunzo hayo Samweli Kinunda na Severine Mbunda, waliwapongeza
wafadhili pamoja na viongozi wa Chama hicho, kwa kuandaa Mafunzo hayo
ambayo yamewasaidia kutambua Changamoto katika zao la kahawa kwa kuwa
awali walikuwa wanalima kienyeji na kupata mazao kidogo yasiyo na
ubora, lakini kwa sasa watatumia mafunzo waliyopewa kuboresha na
kuitunza kahawa na kuipeleka kiwandani ikiwa na ubora wa hali ya juu ili
kujiongezea kipato.
No comments:
Post a Comment