Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha Na Patrick Mabula, TimesMajira Online, Kahama.
WATU wanne wameuawa kikatili kwa kukatwa katwa na kitu chenye ncha kali katika machimbo ya
dhahabu ya wachimbaji wadodo wadogo ya Ntambalale,Kijiji cha Wisolele Kata ya Segese wilaya Kahama baada ya kuvamiwa na kundi watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana diwani wa kata ya Segese, Joseph Manyala, amesema tukio hilo limetoke juzi saa tisa usiku, ambako kundi la watu waodhaniwa kuwa ni majambazi walivamia katika mitambo ya kuchejulia dhahabu kisha kuwaua na kuwapora dhahabu iliyokuwa katika hatua ya uchenjuaji
Manyala amesema watu hao ambao idadi yao haikuweza kufahamika mara moja walivamia eneo hilo saa tisa usiku na kuwaua wafanyakazi wa kituo hicho wanne na mmoja kujeruhiwa vibaya kisha kupora viroba vya madini ya dhahabu vilivyokuwa katika hatua ya uchejuaji.
Amesema kudi la watu hao wanaodhaniwa kuwa ni majambazi baada ya kufika hapo walianza kwa kuwakamata walinzi wawili wa kituo hicho na baadae wafanyakazi wengine watatu na kuwakatakata na kitu chenye ncha kali na kufariki dunia.
Manyala amesema baada ya kuwaua kinyama wauaji hao waliwafungia katika moja ya vyumba vya kituo hicho na kutoweka kusikojulikana. Amesema kutokana na kelele zilizosikika usiku huo wasamaria wema walikwenda katika kituo hicho na kukuta mauaji hayo na kuwataarifu viongozi.
Amesema yeye na wasamaria wema waliokwenda eneo la tukio walikuta miili hiyo ya marehemu hao imefungiwa katika moja ya chumba na kubaini kuwa mmoja alikuwa bado hai na kuanza kumsaidia kuokoa maisha yake.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha alipoulizwa alikiri kuuawa kwa watu hao na mmoja wao kujeruhiwa baada ya kuvamiwa na kundi la wanaodaiwa kuwa ni majambazi kisha kuwakata kata na kitu chenye ncha kali. Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, ACP Joseph Paul amethibisha kutokea tukio hilo na kusema amekwenda eneo la tukio na askari kufanya upelelezi pamoja na kuwasaka watuhumiwa na kuahidi kutoa ufafanuzi baadaye.
No comments:
Post a Comment