Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Mhe.
Gabriel Malata akipokea kompyuta mpakato moja kati ya tano zilizotolewa
na Shirika la Nyumba la Taifa kutoka kwa Meneja Huduma kwa mteja wa
Shirika hilo Bw. Muungano Saguya .ofisini kakwe Jijini Dar es Salaam.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Mhe.
Gabriel Malata akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria
hafla ya makabidhiano ya kompyuta mpakato tano zilizotolewa na
Shirika
nyumba la Taifa (NHC). kutoka kulia kwake ni Meneja Huduma kwa Wateja wa
NHC Bw. Muungano Saguya, Bi. Yumriheri Ndullah ambaye ni Afisa Habari
wa Nhc akifuatiwa na kaimu Mkuu wa kitengo cha manunuzi Ofisi ya Wakili
Mkuu wa Serikali Bw. Emil Emmanuel ktoka kushoto ni Dr. Mussa Abdul
Mkurugenzi wa mipango, Aziz Makaburi ambaye ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
TEHAMA pamoja na Bi. Devota Ngulugulu ambaye ni Mhasibu Mkuu wa Ofisi
ya Wakili Mkuu wa Serikali. ,Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali iliyopo Jijini Dar es Salaam
………………………………………………………………………………………..
Na. Dennis Buyekwa- OSG
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imefanikiwa kuokoa
kiasi cha shilingi Tirioni 11.4 baada ya kushinda mashauri mbalimbali
yaliyoendeshwa katika Mahakama mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Hayo yamezungumzwa mapema leo na
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Mhe. Gabriel Malata alipokuwa akipokea
msaada wa kompyuta mpakato tano zenye thamani ya shilingi milioni 7.5
zilizotolewa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ofisini kwake jijini
Dar es Salaam.
Mhe. Malata ameeleza kuwa kiasi
hicho cha fedha kimeokolewa katika mwaka wa fedha 2019/2020 kufuatia
utendaji mzuri wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambao umepelekea
kushinda mashauri mengi yaliyofunguliwa dhidi ya Serikali.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa fedha
hizo zilizookolewa na Serikali zitasaidia katika kuboresha miradi
mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kama vile ujenzi wa reli ya kisasa
(SGR), ununuzi wa ndege na meli kubwa za abiria na mizigo katika
kuhakikisha tunafikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Amesema kuwa kompyuta hizo
zimekuja muda muafaka kwani zitawawezesha watumishi wa Ofisi ya Wakili
Mkuu Mkuu wa Serikali kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kwa haraka
zaidi hatua itakayosaidia kuongeza ufanisi zaidi katika majukumu yao.
Aidha, Naibu Wakili Mkuu ameongeza
kuwa kompyuta hizo zitakuwa msaada mkubwa kwa Ofisi yake kwa kuzingatia
ukweli kuwa mwaka huu tunaenda kwenye zoezi la uchaguzi hivyo
itawawezesha watumishi wake hususani mawakili katika kutekeleza majukumu
ya usimamizi wa mashauri.
“Mwaka huu tuna jukumu la uchaguzi
na uchaguzi huwa unapelekea kuibuka kwa mashauri mengi yanayofunguliwa
kwa ajili ya kupinga matokeo ya uchaguzi”, alisema Mhe. Malata.
Naye Bw. Muungano Saguya ambaye ni
Meneja Huduma kwa Jamii katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) alisema
kuwa wameamua kutoa msaada huo ili kuwasaidia watumishi wa Ofisi ya
Wakili Mkuu wa Serikali kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha
zaidi hatua itakayopelekea kuendelea kuokoa fedha nyingi ambazo
zingeweza kupotea kutokana na upungufu wa vitendea kazi ofisini hapa.
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
ilianzishwa feburuari 12 mwaka 2018 kwa tangazo la serikali Na. 50 ikiwa
na lengo la kuratibu, kusimamia na kuendesha mashauri yote ya madai
pamoja na Katiba, Uchaguzi na haki za binadamu yanayofunguliwa dhidi ya
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment