Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula kuhusu maendeleo ya
ukarabati wa ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention jijini Dodoma leo. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Joseph Magufuli lamekagua
maandalizi ya kumbi za mikutano na vikao vya chama vinavyotarajiwa
kufanyika hivi karibuni.
Rais Magufuli akiwa ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara),
Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally Kakurwa amekagua
kumbi za Kituo cha Mikutano Dodoma (Jakaya Kikwete Hall) ambako
utafanyika Mkutano Mkuu wa CCM na pia amekagua jengo la Ofisi za Makao
Makuu ya CCM (White House jijini Dodoma).
Pia Rais Magufuli amewapongeza wajumbe wa Sekretarieti ya CCM na
wasimamizi wa ukarabati uliofanyika katika majengo hayo ya CCM ambayo
yanatarajiwa kuwa tayari ifikapo tarehe 20 Juni, 2020.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi, Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Katibu
Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akipita kukagua ukarabati wa
Ukumbi NEC katika Makao Makuu ya CCM White House jijini Dodoma leo. (Na
Mpiga Picha Wetu).
Magufuli amesisitiza kuwa, pamoja na kufanyika kwa mchakato wa
uchaguzi ndani ya chama, Uchaguzi Mkuu lazima utakuwepo na hivyo
amewataka wanachama wote wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za
uongozi kujitathmini na kujiridhisha kama wanatosha kugombea nafasi
wanazoomba.
Ameonya kuwa kuelekea katika mchakato huo wanachama hawana budi
kuweka mbele maslahi ya chama badala ya maslahi yao binafsi na pia
kutofanya vitendo vya kuwagombanisha na fujo ambavyo vitakavyokiumiza
chama.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi, Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Katibu
Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa pamoja na Makamu Mwenyekiti CCM-
Bara, Philip Mangula akikagua kazi ya ukarabati wa maeneo mbalimbali ya
ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention jijini Dodoma leo. (Na
Mpiga Picha Wetu).
Dkt. Magufuli amewataka wana CCM kote nchini kutembea kifua mbele na
kuyasema mambo yote ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa
wananchi, badala ya kuacha jukumu hilo kwa viongozi wachache.
No comments:
Post a Comment