Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai akizungumza na mshindi wa kwanza wa promosheni maalumu inayofahamika kama TAJIRIKA na eGazeti inayoendeshwa na kampuni hiyo. Mshindi huyo amejipatika kitita cha Sh1 milioni. Uzinduzi huo
umefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai akionyesha namba ya mshindi wa kwanza wa Sh1milioni katika uzinduzi wa promosheni maalumu inayofahamika kama TAJIRIKA na eGazeti inayoendeshwa na kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai akizungumza katika uzinduzi wa promosheni maalumu inayofahamika kama TAJIRIKA na eGazeti inayoendeshwa na kampuni hiyo. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau
mbalimbali
Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Ltd, Bakari Machumu akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika uzinduzi wa promosheni maalumu inayofahamika kama TAJIRIKA na eGazeti inayoendeshwa na kampuni hiyo. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Francis Nanai(kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela(kushoto) na aliyeko katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga wakiwa katika uzinduzi wa
wa promosheni maalumu inayofahamika kama TAJIRIKA na eGazeti inayoendeshwa na kampuni hiyo. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
===== ===== =====
Kampuni
ya Mwananchi Communications Limited (MCL) ambao ni wachapishaji wa
magazeti ya Mwananchi, The Citizen, Mwanaspoti na pia watoa huduma
kupitia njia mbalimbali za mtandaoni,
imezindua rasmi promosheni maalumu inayofahamika kama TAJIRIKA na eGazeti.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendani wa
MCL, Francis Nanai, alisema kuwa, promosheni hiyo inalenga kuwazawadia
wasomaji wake, ambao kwa muda mrefu wamekuwa nao tangu kuanzishwa kwa
magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya MCL hadi sasa ambapo unaweza
kuyasoma magazeti mtandaoni kwa urahisi na kwa bei nafuu.
Promosheni
hii inakuja wakati ambapo,huduma ya kusoma magazeti mtaandaoni
iliyopewa jina la eGazeti ikiwa na miezi mitatu lakini kwa muda mchache
tu ina watumiajia zaidi ya 70,000 ndani na nje ya Nchi.
eGAZETI
ni mfumo bora wa kusoma magazeti mtandaoni ya Mwananchi Communications
Limited (MCL). Ili uweze kusoma magazeti mtandaoni unachotakiwa kufanya
ni kupakua App ya eGazeti kwenye Google Playstore au tembelea www.egezeti.co.tz .
Kwa
kutumia mfumo wa eGazeti unayasoma magazeti kutokwa Mwananchi
Communications Ltd kwa urahisi na kwa bei nafuu ikiwemo kifurushi cha
Shilingi1, 000 tu ambacho unasoma nakala ya Mwananchi, The Citizen na
Mwanaspoti.
Gazeti
linapatikana kuanzia saa sita usiku, njia rahisi za kulipia gazeti,
kuchangua vifurushi mbalimbali kadri ya uhitaji wako na eGazeti
inakuwezesha kusoma machapisho hata kama utakuwa ‘offline’ baada ya
kupakua mwanzoni, pia itakuwezesha kuona maktaba yako ambayo
inakurahisishia usomaji.
Zaidi Ndugu Nanani alisema kuwa Tanzania ni nchi kubwa na kwakutumia
Tehama na wabunifu wa hapa hapa ndani ya nchini wameweza kufanikisha
eGazeti na kuwawezesha watanzania kusoma nakala zao popote walipo ambapo
mitando inapatikana. Alisisitiza kila seketa inajukumu la kuwezesha vipaji na wao kama MCL wanafanya hivyo na HabariHub.
Dau Technologies nikampuni ya kiTanzania iliyo tumia fursa za HabariHub na kuweza kubuni na kuboresha mfumo wa kusambaza magazeti kwa njia ya mtandano.
“Tuna
wasisitiza na ku”Promote” vijana wa kitanzania kuwa wabunifu na kutumia
Tekenohama kufanya mapinduzi ya uchumi, hivyo tutaweza kujenga Taifa
letu kuwa imara Zaidi” alisema Mr. Nanani.
Ndani
ya eGazeti utaweza kuchagua na kulipia gazeti kwa: malipo kwa siku,
malipo kwa wiki, malipo kwa mwezi, malipo kwa miezi mitatu na malipo kwa
mwaka mmoja.
Kwa
mujibu wa Mhariri Mtendaji mkuu wa MCL, Bakari Machumu alisisitiza
kuwa, lengo la MCL ni kuhakikisha kuwa wasomaji wa magazeti ya
Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti wanapata habari zilizo bora na
zinazokwenda na wakati na pia zilizofanyiwa utafiti na uchambuzi wa
kina.
Pia
Mkuu wa Idara ya biashara wa MCL, Kenneth Mugabe alisema, katika
promosheni hiyo kutakuwa na zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na zawadi
za kila siku, wiki na za mwisho wa promosheni.
Zaidi
ya milioni 100 zitashindaniwa. Milioni 20 kila mwezi, milioni 5 kila
wiki na Milioni 2 kila siku, Na kubwa kuliko ni 20,000,000/=
atakayoondoka nayo mshindi wa jumla katika droo kubwa ya mwisho wa
promosheni baada ya miezi mitatu.
Droo
za kila wiki zitakuwa zinarushwa kupitia chaneli ya YouTube ya
Mwananchi Digital kila Jumanne saa nne kamili asubuhi kuanzia tarehe 07
June 2020. Katika promosheni hiyo itakayofanyika kwa wiki 12 mfululizo
katika mikoa yote ya Tanzania, msomaji atatakiwa kununua na Kusoma
magazeti ya Mwananchi, The Citizen and Mwanaspoti mtandaoni kupitia
eGazeti kadri awezavyo.
Ili
uweze kusoma magazeti piga 150*48# au Pakua App ya eGazeti kwenye
Google playstore pia waweza kusoma kwa kutembelea tofuti yetu ya www.egazeti.co.tz.
Pointi
ni jumla ya tokeni ulizoingiza katika droo baada ya kunua na kusoma
magazeti. Kadri unavyoongeza pointi, ndivyo unavyojiongezea nafasi ya
kushinda Vigezo na masharti vizitazingatiwa katika droo ya kutafuta
washindi chini ya usimamizi wa na Bodi ya Taifa ya Michezo ya
Kubahatisha.
Machumu
aliwataka watanzania kuchangamkia fursa kupitia promosheni hii na
kusisitiza watu kufatilia na kushiriki maongezi kwenye mitandao yetu ya
kijamii kupitia hashtags #TajirikaNaeGazeti pamoja na #SomaNaUshinde.
Mr
Mugabe alimaliza kwa kutaja gharama za kampeni nzima hii Tajirika na
eGazeti kuwa ni shilingi milioni mia mbili (200,000,000/=).
No comments:
Post a Comment