Mkuu
wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Mhandisi
Lawi Odiero akizungumza kuhusiana na operesheni ya wasafirishaji
vifurushi Katika Kituo cha Mabasi Ubungo jijini Dar essalaam.
Mfanyakazi
wa Kampuni ya kusafirisha vifurushi kwa njia basi Ya M Cargo akiwa
ameshikiliwa na Polisi katika Operesheni yaTCRA ya kuwasaka
wasafirishaji wa vifurushi wa sio na leseni katika kituo Cha mabasi
Ubungo.
Msafirishaji
wa vifurushi wa kampuni ya Suti Africa Gisela Paulo akitoa maelezo ya
kuwa hausiki na usafirishaji huo wakati alijaza fomu ya usafrishaji.
Emmanuel
Cornel akitoa maelezo namna ya changamoto iliyomkuta wakati
aliosafirisha kifurushi ambapo Hadi tarehe 29 mwezi huu mlengwa
hajifikiwa na huduma hiyo.
Baadhi ya vifurushi vinavyosafirishwa na kampuni ya M Cargo Transport.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAMLAKA
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imefanya operesheni
kwa kampuni yanayosafirisha vifurushi bila kuwa na leseni kutoka
katika mamlaka hiyo hali ambayo inaleta usumbufu kwa wananchi pale
wanapokuwa wametuma vifurushi hivyo.
Akizungumza
na waandishi habari wakati wa operesheni hiyo Mkuu wa Kanda ya
Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero amesema operesheni hiyo ni
endelevu kwa kampuni zinazosafirisha vifurushi bila ya kuwa na leseni
hali ambayo inasababisha serikali kukosa mapato.
Amesema
kuwa operesheni hiyo wanaifanya kwa kushirikiana na jeshi la polisi
ambapo baada ya kuwakamata wasafirshaji hao wanafunguliwa mashitaka ya
kufanya biashara ya usafirishaji vifurushi kwa njia ya basi bila kuwa
na leseni
"Hii
ni operesheni endelevu kwa wasarishaji vifurushi bila kuwa na leseni
nia ni kutaka wafanyabiashara ya usharishsji wa vifurushi wafuate
matakwa ya sheria kwani kazi hiyo wanaiokosesha serikali mapato"amesema
Odiero.
Aidha
amesema kuwa utaratibu wanaohitaji leseni upo wazi hivyo kwa wale
wanaohitaji wafuate sheria na kama wataendelee kutoa huduma hiyo bila
kuwa leseni sheria itashika mkondo wake.
Kampuni
zilizokuwa zikifanya biashara ya kusafirisha vifurishi bila ya kuwa na
Leseni ni M CargoTransport, pamoja na Suti Afrika katika kituo cha
mabasi ubungo.
Aliyekamatwa
wa Kampuni Suti Afrika Gisela Paulo amesema kuwa yeye sio wa kampuni
hiyo alichokifanya ni kujaza fomu ya kusafirishia mzigo kwani kampuni
hiyo wako katika ofisi moja hakujua kama hawana leseni.
Mmoja
ya wananchi aliyepata huduma M Cargo Transport Emmanuel Cornel amesema
kuwa alipata huduma ya kusafirsha kifurishi lakini hadi leo hakijafika
huku hakuna majibu sahihi ya nani alipokea fedha kwa ajili ya
usafirshaji wa kifurushi.
No comments:
Post a Comment