Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa katika mazungumzo na Balozi wa
Taifa la Israel kwa Tanzania Mhe. Oded Joseph ambaye analiwakilisha Taifa hilo kutokea Nairobi, Kenya.
Kanali Balozi Ibuge katika mazungumzo hayo amweleza Balozi Oded,
kuhusu hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kukakabiliana
na kusambaa kwa COVID-19 na madhara sambamba na madhara cake.
Aidha, pamoja na mambo mengine Wawili hao katika mazungumzo yao
wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo ya kuendelea kukuza na kudumisha
uhusiano wa kidiplomasia na biashara baina ya Tanzania na Israel. |
No comments:
Post a Comment