Pages

Friday, May 1, 2020

SERIKALI YAKANUSHA VIFO VYA WATU 50 DAR KWA CORONA



……………………………………………….
Na.Alex Sonna,Fullshangwe
Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Dkt.Hassan Abbasi ameikosoa vikali televsheni  NTV Kenya na kusema wamechapisha taarifa za uongo baada ya kudai kuwa kwa siku ya jana April 30,2020 pekee wamefariki Watu 50 katika Mkoa Dar es Salaam  kutokana na corona.

Kupitia akaunti yao ya Twitter NTV waliweka taarifa inayosema idadi ya watu wanaokufa kwa
ugonjwa wa Corona jijini Dar es Salaam kwa siku ni 50 jambo ambalo Dk Abbas amelikanusha akisema ni uongo.
” Watu 50 wanakufa kwa siku jijini Dar es Salaam kwa maambukizi ya Corona, Kiongozi Mkuu wa Upinzani Tanzania siku ya Jumatano aliishutuma serikali kwa kuficha taarifa sahihi za ugonjwa huo na kushindwa kuchukua tahadhari ya kudhibiti maambukizi,” Hii ndio taarifa iliyowekwa na NTV kwenye mtandao wao wa Twitter.
Sasa baada ya taarifa hiyo kusambaa, Dk Abbas ameishutumu NTV kwa kuripoti taarifa hiyo ambayo siyo sahihi huku akiwakumbusha kufuata misingi ya taaluma ya habari.
” Huu ni Uandishi au Uhandisi wa habari? Inasikitisha kuona jinsi NTV Kenya inavyokua wakala wa uongo na uzushi. Nawakumbusha wazandiki hawa kuenzi misingi ya taaluma badala ya umaamuma,” Imesomeka hivyo taarifa ya Dk Abbas aliyoiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Ikumbukwe jukumu la kutoa taarifa ya maendeleo ya ugonjwa wa Corona inatolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa au Rais Dk John Magufuli.

No comments:

Post a Comment