Pages

Saturday, May 30, 2020

RAIS MAGUFULI AWAKABIDHI MARAIS WASTAAFU TAUSI 25 KILA MMOJA NA MAMA MARIA NYERERE KWA KUTAMBUA MCHANGO WAO KATIKA TAIFA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Hati ya Makabidhiano ya zawadi ya Ndege aina ya Tausi 25 kwa Mama Maria Nyerere mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kuwafuga katika Makazi yake, hafla hiyo fupi ilifanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla ya Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla ya Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi 25 kwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuwafuga katika makazi yake. Hafla ya Makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi hao Wakuu wastaafu mara baada ya kuwakabidhi zawadi ya ndege aina ya Tausi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika hafla hiyo fupi ya Makabidhiano ya zawadi ya ndege aina ya Tausi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakati akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya Marais wenzake wastaafu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya hafla fupi ya Makabidhiano ya ndege aina ya Tausi katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa. 
PICHA NA IKULU
………………………………………………………
Na.Alex Sonna, Chamwino
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewakabidhi Marais Wastaafu wa Tanzania kila mmoja Tausi 25 wanaopatikana Ikulu, ili wakawatunze kwenye
bustani zao, Mama Maria Nyerere amekabidhiwa pia Tausi hao kwa niaba ya Baba wa Taifa Mwl. Nyerere.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma katika makao makuu ya Nchi.
”Tanzania hatukuwahi kuwa na Tausi waliltetwa na Baba wa Taifa, Mama Maria anaifahamu zaidi historia yake, Mzee Mwinyi aliwakuta angeweza kuwachinja na kuwala nyama maana nyama yake tamu kuliko kuku ila aliwatunza, Mzee Mkapa na Kikwete pia wakawatunza”Amesema Rais Magufuli
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa amekabidhi ndege hao kama sehemu ya kutambua mchango wao katika taifa hili .
Hata hivyo Rais Magufuli amesema kuwa Wakati Mzee Kikwete anakabidhi Ikulu alimwaambia Tausi hawa wanataga mayai vizuri ila hawayalalii yanaliwa na wanyama, kuna mfanyakazi hapa tena msukuma mwenzio kila nikimuambia atafute incubator atotoe mayai hafanyi, nilipoingia yule Msukuma nikamfukuza.
”Nimeingia Ikulu nikaleta wataalamu wa wanyama tukanunua incubator idadi ya mayai ya Tausi ikaongezeka, nimetoa Tausi 100 kila Mstaafu Tausi 25 ili wakawaburudishe wajione kama wapo Ikulu, nikajua atakuja mmoja siku moja atawanyang’anya, nimesaini na hati”-Ameeleza Rais Magufuli
Pia Rais Magufuli amesema kuwa Tausi hawa ambao kila Rais Mstaafu nimemkabidhi 25 wataanza kuondoka leo hii tumeshaandaa utaratibu kuwasafirisha kwenda Butiama, Msoga nk, ikitokea mmoja akafia njiani tutareplace.
Mbali na kukabidhi Tausi hao Rais Magufuli pia ametoa kilo 100 za chakula cha Kuanzia Kwa tausi hao pale watakapokuwa wamewasili katika bustani za viongozi hao.
Naye Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa neno la shukrani kwa niaba ya marais wastaafu amesema kuwa wanashukuru sana kwa upendo, ukarimu, na wanampongeza namna anavyoendeleza kijiti kwa kufanya mambo makubwa katika nchi hii .
Ikumbukwe Wakati Rais Magufuli anaingia Ikulu aliwakuta Tausi 403 lakini kwa kazi kubwa aliyofanya ya kuwatunza, kwa sasa Tausi wamefikia 2260 katika Ikulu ya DSM, hapa Ikulu ya Dodoma kuna Tausi 544 na wapo wengine wamepelekwa kwenye Ikulu za Mikoani

No comments:

Post a Comment