Chama
cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA kimetoa maelekezo kwa Wabunge wake
wote, kutohudhuria tena vikao vya Bunge vinavyoendelea,na wajiweke
Karantini kwa muda wa siku 14 na wasiende majimboni kwao kipindi hiki
mpaka pale watakapothibitika hawana maambukizi ya Virusi vya Corona.
Taarifa
iliyotolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe leo Ijumaa May
1, 2020 imetoa maelekezo manne kwa wabunge wa chama hicho ambayo ni;
Kutohudhuria vikao vya bunge au kamati za bunge,Kutofika eneo la Bunge
Dodoma na Dar es Salaam, Wabunge wajiweke karantini kwa muda wa siku 14,
wabunge wa chama hicho wasiende mikoani au majimboni bali wabaki Dodoma
hadi itakapothibitika hawana maambukizi
Aidha, CHADEMA pia wameshauri Bunge
lisitishwe kwa siku 21 ili kuruhusu wabunge wote kwenda Karantini,
Wabunge wote wapimwe pamoja na familia zao na Kamati za Bunge zifanye
vikao kwa njia ya mtandao
No comments:
Post a Comment