Wafanyakazi wa hotel ya Naura Springs na Impala hotel pichani wanaodai mishahara yao |
Wafanyakazi
wa Hotel za Impala na Naura Springs wanasotea mishahara yao tokea Mwezi
wa Tisa mwaka jana huku uongozi wa kampuni hizo ukidai kuwa hauna fedha
kutokana na Ugonjwa wa Covid 19.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wafanyakazi hao ambao wapo majumbani na wengine
kazini wakisotea mishahara yao bila kulipwa kwa zaidi ya miezi nane
huku Mkurugenzi mbele ya waziri akiahidi kuwapa mishahara yao January 31
mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Naibu waziri wa kazi ajira na watu wenye ulemavu Anthony
Mavunde kwenye kikao chake na wafanyakazi wa hotel hizo na Mkurugenzi
wao Randle Mrema walikubaliana kuanza malipo mnamo Mwezi wa January 2020
jambo.ambalo halijatekelezwa hadi leo hii.
“Ndugu
mwandishi sisi tunaishi maisha ya kuomba omba wakati tuna mikataba ya
kazi huku kwenye majumba tuliopanga tunadaiwa Kodi huku wengine wakiwa
wamefukuzwa katika majumba hayo wengie ni wagonjwa hawajui kesho yao
kutokana na kukosa malipo hayo aliyoahidi Mkurugenzi wetu mbele ya
waziri wa kazi kuwa atatulipa kila mwezi kama kawaida”alisema Sia Lyimo
Kwa
Upande wake Kiongozi wa wafanyakazi hao wa Impala group Lyimo alisema
kuwa yeye amekuwa akipata lawama nyingi kutoka kwa wafanyakazi wenzake
baada ya makubaliano ya awali mbele ya waziri kutotekelezwa hadi sasa
Jambo linalowawia vigumu kujua hatma yao ni ipi.
Kwa
mujibu wa wafanyakazi hao wanaodai malimbikizo ya mishahara ya miezi
nane Sasa wamemuomba Rais na Serikali yake kuingilia kati sakata hilo
ili waweze kupata haki na stahili zao kwani viongozi wa Serikali mkoa na
wilaya wameshindwa kuwatendea haki kupata haki zetu huku tukiwa na
mashaka nao.
Kwa
nyakati tofauti huko nyuma Mkurugenzi wa Impala group of Companies
Randle Mrema amekuwa akidai kampuni hiyo ikiwa kwenye hali mbaya ya
kifedha na watajitahidi kuwalipa fedha zao ndani ya muda Jambo ambalo
ameshindwa kulifanya.
Alipotafutwa
kwa njia ya simu kujibu tuhuma hizo Randle Mrema simu yake
haikupatikana kwa wakati wote na Juhudi zinaendelea ili kuweza kujibu
tuhuma hizo za kushindwa kuwalipa mishahara kwa miezi minane Sasa.
No comments:
Post a Comment