Pages

Wednesday, April 29, 2020

SIMIYU INA FURSA YA KUZALISHA MAZAO MENGI YA BIASHARA



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka (aliyesimama) akiongea  na Katibu Mkuu  Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ( aliyekaa kulia) wakati wa kikao cha wadau wa zao la pamba mjini Simiyu leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akinawa mikono kwa maji na dawa alipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuanza ziara ya kukagua shughuli zinazofanywa na wizara ya kilimo 
Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( aliyevaa tai) akitoa maelekezo kwa  Maj.E. Buberwa msimamizi wa mradi wa ujenzi wa jengo la wizara ya Kilimo katika viwanja vya Nane nane Nyakabidi Bariadi mkoani Simiyu 
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (aliyeshika dumu ) akitazama bidhaa za mafuta yanayozalishwa na kiwanda cha kuchambia pamba cha NGS Bariadi mkoa wa Simiyu leo 
Picha na Habari na Wizara ya Kilimo.
************************************
Wizara ya Kilimo imewataka wananchi wa Mkoa wa Simiyu kuongeza uzalishaji wa zao la pamba sambamba na mazao mengine mengine ya biashara ili kuwa na uhakika wa mapato.
Kauli hii imetolewa leo mjini Bariadi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya wakati aliopongea na wanunuzi wa zao la pamba katika kikao kilichofanyika ofisini kwa Mkuu wa Simiyu.
Katibu Mkuu huyo amewasihi viongozi wa mkoa wa Simiyu kuwahamisha wakulima pamoja na kuzalisha
zao la pamba watumie ardhi iliyopo kuzalisha zao la mkonge na korosho yanayoweza kustawi vizuri
kwenye mkoa huu.
“ Nawashawishi wakulima wa Simiyu pamoja na kulima pamba kwa wingi pia walime mkonge pia kwani
tunacho kituo chetu cha TARI Mlingano chenye uwezo wa kuzalisha na kusambaza mbegu bora za
mkonge hadi hapa.” Alisisitiza Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo.
Kusaya amesema anatambua uwepo wachangamoto za madai ya baadhi ya wakulima wa zao la pamba
pamoja na halmashauri kutokana na ushuru kutolipwa na kuwa serikali itafikia suluhu ya jambo hili.
Amewataka wanunuzi wa zao la pamba kuendelea na maandalizi ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza
mwanzoni mwa mwezi Mei na kuwa serikali inaendelea kushughulikia madai hayo.
Kusaya alisema ifike wakati kama kulikuwa na makosa yalifanyika huko nyuma kuhusu msimu wa pamba
sasa lazima tuangalie wanunuzi na serikali tumejiandaa namna gani.
“Ifike mahala kama kuna makosa tuliyafanya huko nyuma yasiathiri uuzaji wa pamba ya wakulima kwani wana imani sana na serikali ya Awamu ya Tano.Ndio maana nimetembelea mikoa hii ya Simiyu,Shinyanga na pia nitaenda Mwanza kujionea hali ya maandalizi ya msimu wa pamba” Kusaya.
Katika kikao hicho Kusaya aliwaomba viongozi wa mkoa wa Simiyu na wa Chama cha Mapinduzi kushirikiana wizara ya Kilimo kutengeneza mazingira mazuri ya wakulima kuendelea kunufaika na kazi zao kwa kupata soko la uhakika .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka alisema mkoa wake ndio unaoongoza
nchini kwa uzalishaji wa pamba na kuwa wakulima wana imani na serikali katika kuhakikisha wanapata
fedha zao zilizosalia.
Mtaka aliyataja kiasi cha Shilingi Bilioni 3.5 bado hakijalipwa kwa halmashauri za mkoa wake kama
ushuru wa mazao kutoka kwa wanunuzi na kiasi cha Shilingi Milioni 794 kinadaiwa na wakulima hadi
sasa.
Mkoa wa Simiyu katika msimu wa mwaka 2018/2019 ulizalisha kilo milioni 166.19 za pamba na kuufanya
ushike nafasi ya kwanza kitaifa.

No comments:

Post a Comment