Pages

Wednesday, April 29, 2020

COCACOLA YAIUNGA MKONO TANZANIA REDCROSS


************************************
Tanzania Red Cross Society leo imepokea hundi ya sh. Milioni 230 kutoka katika kampuni ya Cocacola Tanzania ikiwa ni mchango wa kuunga mkono shughuli zinazofanywa na
Tanzania Red Cross katika kukabiliana na Virusi vya CORONA.
Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Tanzania Red Cross Mikocheni, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Cocacola Tanzania Ndg Halid Mzee Ali amesema kuwa Cocacola imeamua kuunga mkono Tanzania Red Cross Society kwakua Red Cross ni ya wote na imepewa mamlaka na serikali kushughulia janga hili nchini.
Nae Katibu Mkuu wa Tanzania Red Cross Society Ndg Julius Kejo ameishukuru kampuni ya Cocacola Tanzania na wadau wengine kwa kutambua na kuunga mkono kazi zinazofanywa na Tanzania Red Cross katika kukabiliana na Virusi vya Corona.
Aidha, Balozi wa Kampuni ya Cocacola na Tanzania Red cross Society Mrisho Mpoto amehamasisha wananchi katika ngazi zote kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa Covid-19 na kutoa kauli mbiu yake kwa watanzania inayosema “Nguvu yetu ni maji na sabuni”.

No comments:

Post a Comment