……………………………………………………………………………………………
Na Bashiri Salum,Wizara ya Kilimo
Morogoro
Tume ya Umwagiliaji nchini
imetakiwa kujikita katika miradi michache itakayo kamilika na
kuleta
tija kwa wakulima kuliko kuwa na miradi mingi isiyokamilika.
Katika kipindi cha miaka mitano
kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020 mkoa wa Morogoro imekuwepo miradi saba
inayotekelezwa katika wilaya Zaidi ya 11 ambapo mingi haijakamilika
kutokana na changamoto mbalimbali.
Akiongea na wahandisi wa Tume
hiyo katika ofisi ya kanda iliyoko Morogoro Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo Bw. Gerald Kusaya ameishauri Tume hiyo kuwa na miradi michache
ambayo itakamilika kwa ufanisi mkubwa.
Amesema Tume ya Umwagiliaji kwa sasa ina deni kubwa kwa wakulima na wananchi kwa ujumla ambao wamepoteza Imani na tume hiyo.
“Fanye kila litakalowapendeza
mhakikishe mnarudisha Imani kwa wananchi na Raisi wa Jamhuri ya
muunganoo wa Tanznania Mhe. Dkt John pombe magufuli” alisema Bw. Kusaya.
Akitolea mfano wa skimu za
umwagiliaji za Kilangali, Msola Ujamaa na Kigugu amesema matatizo ya
skimu hizi yametokana na usimamizi usioridhisha na kutochukuwa hatua kwa
wakandarasi hivyo kusababisha wakulima kushindwa kufikia malengo yao.
Aidha Katibu Mkuu amewataka
wahandisi hao kufanya kazi kwa ushirikiano na kujiamini wakati
wakitambua kuwa Tume inamchango mkubwa katika kubadilisha Maisha ya
wakulima na taifa kwa ujumla.
Hata hivyo Bw. Kusaya ameitaka
tume kuyatangaza mambo mazuri wanayoyafanya kupitia vyombo vya Habari
ili wadau waweze kuifahamu tumena kwa kuwa mambo mengi yanatokana na
kutokuwa na taarifa sahihi.
Awali akitoa taarifa kwa Katibu
Mkuu na viongozi wengine walioambatana nao Kaimu Mhandisi umwagiliaji
mkoa wa Morogoro Njanji Mlwale amesema changamoto ya ukosefu wa fedha
kulingana na mahitaji umechangia kwa kiasi kikubwa miradi mingi kuto
kamilika.
Mhandisi Njanji amebainisha kwamba
umekuwepo mgongano wa utekelezaji wa majukumu baina ya Tume na
wataalamu walioko chini ya wakurugenzi watendaji wa Halmashauri
mabalimbali ambao wanatekeleza shughuli za umwagiliaji kama ilivyo Tume.
Muingiliano huo wa majukumu
umekuwa ukisababisha miradi mingi ya Halmashauri kutokamilika na lwama
kurudi kwa Tume ya Taifa ya umwagiliaji alisema Mhandisi.
Hata hivyo Mhandisi Njanji
amebainisha kwamba ukosefu wa maabara ya Tume ambayo ingesaidia katika
vipimo mbalimbali imesababisha uchelewashaji wa miradi kwa kuwa Pamoja
na kugharimu fedha nyingi lakini sampuli zimekuwa zikichelewa .
No comments:
Post a Comment