Pages

Monday, March 2, 2020

RAIS DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA UJENZI MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI ZANZIBAR. IKULU JIJINI ZANZIBAR



RAIS wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein , akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar, wakati wa kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa Wizara hiyo kwa  mwezi wa Julai  hadi Disemba 2019 , mkutano uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, (kulia kwa Rais) Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi. Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na Waziri wa Ujenzi  Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Dr. Sira Ubwa
BAADHI ya Wakurugenzi wa Idara na Mashirika mbalimbali yal Wizara hiyo wakifuatilia  uwasilishwaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, mkutano uliofanyika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani)
WAZIRI wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Dr. Sira Ubwa akisoma muktasari wa taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yake kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 /2020, mkutano uliofanyika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, (kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi. Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.
KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliani na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud Jumbe, akisoma Taarifa ya Utekelezaji  ya Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019/2020, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
MKURUGENZI Idara ya Usafiri na Leseni  Zanzibar. Ndg. Suleiman Konoo Kirobo, akijibu swali wakati wa Mkutano wa  kuwasilisha taarifa ya utekelezaji mpango Kazi kwa mwezi Julai hadi Disemba 2019 /2020, kiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa  Ikulu Jijini Zanzibar.
BAADHI ya Maofisa wa Idara na Mashirika ya Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji wakifuatilia uwasailishwaji wa utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo ukiwasilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud Jumbe,(hayupo pichani) mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
KATIBU wa Bodi ya Usafiri Zanzibar Ndg. Mohammed Simba Hassan, akijibu swali liliolizwa wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019/2020, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein. (hayupo pichani) 
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini (ZMA).Capt. Abdalla Hussein Kombo, akijibu swali wakati wa mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji ya Mpango kazi kwa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, (hayupo pichani) 
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndg. Abdalla Juma, akijibu swali wakati wa mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019/2020 , ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani)  uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment